Barua kwa Rais Magufuli kuhusu ajira

Jimmy George

JF-Expert Member
Nov 28, 2016
1,733
1,648
Kwako Mheshimiwa Rais,

Kwanza kabisa nakupongeza kwa kazi nzuri unayoifanya ya kuongoza taifa hili la Tanzania na pia pole kwa majukumu uliyonayo,kuna mengi mazuri unayafanya huenda sisi watanzania wa kawaida hatuyaelewi na kuona unakosea ila naamini mwisho wa siku tutaelewa.

Lengo la ujumbe huu kwako ni kuhusiana na kilio tulichonacho sisi vijana ambao kwa muda sasa tunasubiri ajira. Ni muda wa miezi 9 umepita tangu uliposema mbele ya vyombo vya habari kuwa zoezi la uhakiki litadumu mwezi mmoja na nusu haitozidi miwili utakuwa umetoa ajira ambapo wengi tukawa tuna matumaini kuwa zitatoka ajira zile 71,000 lakini mpaka leo kwa taarifa mzitoazo ni kuwa mmetoa ajira 5000 kuachia mbali za wakurugenzi na wenyeviti wa taasisi mbalimbali.

Si kweli kwamba vijana wote ni wavivu na tumeshindwa kujiongeza la hasha kinachopelekea tuonekane wazembe, hatuwezi kujiongeza,mizigo kwa wazazi,hatutaki kujiajiri sababu kubwa ni hizo ahadi zenu mnazotupa za miezi miwili miwili zinafanya tuwe na matumaini makubwa na kungoja ahadi maana hii serikali tunaiamini sana katika utekelezaji wa mambo.

Kutotolewa kwa ajira mpaka sasa kumepelekea hata wazazi wetu waliokupenda sana wakati wa kampeni,kubishana kuwa wewe ni bora kuliko wengine na hata kuimba sana ule wimbo wa waisome namba wameanza kukuchukia kwa sababu walitoa ada zao, gharama zao ili kuwasomesha watoto wao ili wakipata kazi basi waendeleze familia na kuwasaidia ndugu zao. Imepelekea hata kuchukia kauli zako pale wanapolalamika hela hakuna mtaani,imepelekea kuona kila ukisemacho kama hakina maana kwao na sisi vijana kuona serikali hii haitujali tena.

Ombi langu kwako Mheshimiwa Rais Magufuli ni kuwa tuambie ukweli ni lini umepanga kutoa ajira hata kama ni baada ya mwaka huu kuisha au miaka miwili mbele tutaumia ila itatusaidia kujipanga vyema na kamwe hutosikia tukilalamika kuhusu ajira. Chondechonde kupitia mawaziri wako naomba msitupe ahadi tamu za kuwa ajira zitatoka baada ya muda mfupi wakati mipango ya serikali si kutoa ajira mapema.

Sina mengi kwa leo naomba nikutakie kazi njema na uendelee vyema na majukumu yako ya ujenzi wa taifa letu.

Ni mimi mwananchi wako mtiifu,
Jimmy George.
 
People's power
Ndugu wananchi tumekuwa tukipambana ktk kuikomboa Tanzania kiuchumi, kisiasa na Kijamii.
Watanzania wenzangu ni muda wa mabadiliko. Tanzania tunakabiliwa na maadui 4 wa maendeleo nao ni ccm, ujinga, maradhi na umasikini.
-Wananchi ccm ni mzigo na kimeshazeeka na hakifao kuwepo madarakani.
Angalien watoto wenu mnaowategemea wamefutiwa ajira, je huyo raisi ana nia ya dhati kweli kuikomboa Tanzania? Chagua Chadema kwa Maendeleo yenu
Ajira za serikali zitakuwa zinatolewa mwezi wa 1 kwa kila mwaka tutaajiri watu weng sasa. Mkichagua Ccm mtabaki hiv hiv hakuna ajira. Huyo mnayemsifiwa kafuta ajira na hatoajiri. Nani kaajiriwa mpaka sasa?
-Suala la mikopo kwa wanafunzi limekuwa ni kilio, watoto wengi wanatoka ktk familia za chini. Onen watoto wenu wapo nyumbani sasa hivi na wamekosa mwelekeo kbsa. CHADEMA TUTATOA 50% KWA KILA MWANAFUNZI ANAYEINGIA CHUONI
-Suala la HELSB 15% tutarudisha ktk asilimia za mwanzo 8% na hii italeta haueni kwa wafanyakazi.
PEOPL'S POWER
Jaman ndugu wananchi increment zenu meshapewa? Nilishangaa sana watu weng bado wanakimbizana na chama kilichozoeeka na chenye mawazo ya kimasikini. !eo hii ni october 25, 2019 bado hamjapewa increment, hamjapandishwa madaraja. Polen sana kwa uhakiki wa wapiga dili wa ccm. CHAGUA CHADEMA KWA MAENDELEO YAKO
Walimu poleni sana kwa kupigishwa deki, huu uuonevu mnabid muukomeshe kwa kuichagua chadema. People's power
Huyo mliyemchagua kafanya nn mpaka sasa hivi?
Suala la vyeti feki siyo kama tunashabikia ila tunataka haki itendeke. Iweje wengine wafukuzwe lkn yy alindwe.
Ona sasa sukari mnanunua 1 kilo kwa 3,000.
Wanakagera mpoooooooooooooooooooo
"BILA KUMUONDOA ADUI WA MAENDELEO CCM MTAENDELEO KULIA KILA SIKU. HUYO MSEMA KWELI MPENZ WA MUNGU MBONA KADANGANYA UMMA? MWEZI MMOJA AU MIWILI UNA SIKU NGAPI? WATANZANIA MEJICHANGANYA SANA NA HII DHAMBI ITAWATAFUNA MPAKA KESHO KUTWA.
Najaribu tu Wala usiogope mwanaccm. 2019 itakuwa poa sana.
 
Umeshasema anafanya mazuri hata kuzuia ajira ni mazuri utakuja kugundua baadae ni mazuri kama ulivyosema!!! Kinacholimaliza hili taifa ni unafiki unafiki tu na si kingine!!!
Mengine anayoyasema huwa hayana ukomo kuwa ni lini lakini hili la ajira ni danadana laiti angesema kuwa hatutoi zaid ya mwaka mmoja au miwili tusingepiga kelele maana tungejua pia ni jambo jema kinachoumiza ni ahadi zisizotimizwa kwa wakati uliohaidiwa.
 
Sawa umeeleweka mkuu.
Usitegemee utaoata ajira kwa serikàli ya ccm.. Atakwambia nenda ukalime Mashamba hapo mengi
Daaaah inauma sana.
Suala la bashite wa koromije ni muhimu Ndugu yangu, kuna mama juzijuzi amehukumiwa kwenda jela miaka 28 kwa kosa la vyeti feki
Ni kweli haki inapaswa kutendeka.
 
Endelea kuvuta subira kijana, viwanda vinakuja.........usiniulize lini maana namimi nasikia tu wakisema Tanzania ya viwanda.
Umenifanya nicheke km mazuri. Nchi ya viwanda teh teh
KUNA WATU MATAPELI DUNIA HII. WATANZANIA WAKATAPELIKA. MWENYE AKILI TIMAMU HAWEZI KUAMIN SERA ZA CCM HATA KIDOGO
 
Endelea kuvuta subira kijana, viwanda vinakuja.........usiniulize lini maana namimi nasikia tu wakisema Tanzania ya viwanda.
Hahahahahaha
Ahadi tamu za uongo zinaendelea hadi leo wamekuja na hii:
Wanafunzi huwa wanaanzia sekondari kumbe hawatoki shule za msingi maana naona wako busy na walimu wa sayansi wa sekondari wakati shule za msingi hamna daaaah....
 
Wewe unaonekana hujailewa vizuri Sera ya Serikali hii, kuwa mjasiriamali
hivi bado kuna watu wana dhani kuni viongozi wanao wafikiria? kifupi hatuna watu wanao tuongoza, wote wanafikiria familia zao tu basi. ndio maana wana hangaika na Lema na TUNDU LISU as ni magaidi, kumbe wanacho fanya ni kuona kuwa watu hawa hawapigi kelele kuonesha ubaya wao.
 
Power
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…