Barrick Gold Mine yanaswa ukwepaji kodi wa kutisha

Ghadafi alitaifisha makampuni yote ya kuchimba mafuta kwa sababu hizihizi na wananchi walifaidi cake yao ikafikia hatua hata wakawa wanapewa na mshahara.
Nashauri haya makampuni yafilisiwe tuchimbe madini yetu wenyewe ili tupate pesa za kuendesha miradi yetu, make hawa jamaa ni wezi haiwezekani tuwe nchi ya tatu kwa kutoa dhahabu Africa lakini bado tunaombaomba misaada.
Jiongeze kidogo mkuu anayekuibia ndio anayekupa msaada. Kwahiyo mnaposhabikia tupewe misaada mnajenga mazingira ya kuendelea kuibiwa.
 
Hivi madudu yote yanayoibuliwa sasa wanasema kichocheo chake ni 'uthabiti' wa uongozi wa juu wa nchi na sio watendaji wa chini.
Je, tuna haja ya kujiuliza kuwa wakati haya madudu yanatengenezwa ilikuwa sababu ya udhaifu wa uongozi au uongozi wenyewe ulisimamia kuyatengeneza!?
 
Unadhani ukwepaji huo wa kodi ulifanyika miaka gani? Wewe ndio utakuwa umekosa weledi na upumbavu unakuandama.

Ndio maana nikasema hapo juu, unajua ni aina gani ya kodi inayozungumziwa, na mchakato wa kulishughulikia umeanza lini, laiti ungekuwa unajua mambo ya madini na sheria zake, hata usingemlaumu JK katika hili.
 
Kwani hii kesi ilifunguliwa lini ? inawezekana mchakato ulianza zamani kidogo, kwa sababu hapo kuna process zimepitia kabla ya hayo maamuzi
Hiyo statement haionyeshi kesi ilifunguliwa lini, inaonyesha tu kuwa toka 2010-2013 hawa jamaa hawakupata hasara kama walivyokuwa wakidai.
Unless kama una details za lini kesi ilianza.
 
Hiyo statement haionyeshi kesi ilifunguliwa lini, inaonyesha tu kuwa toka 2010-2013 hawa jamaa hawakupata hasara kama walivyokuwa wakidai.
Unless kama una details za lini kesi ilianza.

Wewe kidogo una weledi, unafahamu nini kilijiri, JK hastahili lawama, kama ukizijua kodi za madini na sheria zake.
 
Ndio maana nikasema hapo juu, unajua ni aina gani ya kodi inayozungumziwa, na mchakato wa kulishughulikia umeanza lini, laiti ungekuwa unajua mambo ya madini na sheria zake, hata usingemlaumu JK katika hili.
Wewe uliye na weledi wa kutosha;
1. onyesha ni lini kesi ikifunguliwa?
2. Ni aina gani ya kodi inadaiwa hapo?
2. Kwa nini JK asihusike wakati haya yametokea wakati wa utawala wake? Nielimishe...
 
Wewe uliye na weledi wa kutosha;
1. onyesha ni lini kesi ikifunguliwa?
2. Ni aina gani ya kodi inadaiwa hapo?
2. Kwa nini JK asihusike wakati haya yametokea wakati wa utawala wake? Nielimishe...

Hii kodi inaitwa corporate tax, yaani unaanza kuilipa baada ya kurudisha hela zako za uwekezaji. Sasa kilichofanyika ni kwamba, mahesabu ya uwekezaji ndio yameanza kufanyika miaka ya mwishoni mwa utawala wa JK, na mpaka sasa ndio imefahamika jamaa walisharudisha hela yao ya uwekezaji, tangia muda huo, sasa ndio wanatakiwa kulipa. Kumbuka haya mahesabu hayatoki hvhv, mpaka baada ya kipindi flani. Nadhani umenielewa
 
Hiyo statement haionyeshi kesi ilifunguliwa lini, inaonyesha tu kuwa toka 2010-2013 hawa jamaa hawakupata hasara kama walivyokuwa wakidai.
Unless kama una details za lini kesi ilianza.
ok, sina details , hila inawezekana hiyo kesi ilianza katika utawala wa mkwere, kuna process kama tatu kama sijakosea hiyo hapo ndiyo final stage, ss kwa kuwa kesi za bongo uchukua muda mrefu, ndio maana nikawa na wasi wasi huo, Pia nafikiri kuna room ya kwenda court of appeals
 
Hii kodi inaitwa corporate tax, yaani unaanza kuilipa baada ya kurudisha hela zako za uwekezaji. Sasa kilichofanyika ni kwamba, mahesabu ya uwekezaji ndio yameanza kufanyika miaka ya mwishoni mwa utawala wa JK, na mpaka sasa ndio imefahamika jamaa walisharudisha hela yao ya uwekezaji, tangia muda huo, sasa ndio wanatakiwa kulipa. Kumbuka haya mahesabu hayatoki hvhv, mpaka baada ya kipindi flani. Nadhani umenielewa

Bado sijaelewa, corporate tax inalipwa wakati gani? Kwa nini serikali haikufanya uhakiki wa kimahesabu kila mwisho wa mwaka kujua nini wameingiza, matumizi, faida/hasara ili wajihakikishie uhalali wa hasara/faida kampuni inayopata? Serikali inaweza kuingilia mahesabu ya shirika/kampuni yoyote, una maana gani ukisema sio rahisi kupata hayo mahesabu?
Nielimishe...
 
Kukwepa kwepa ni mwiko siku hizi,ukiiba fedha za uma hatutakuita FISADI tutakuita MWIZI.
 
Isiwe tabu. Katika miaka hiyo yote ambayo hawakuilipa serikali yetu kodi wakati wanapata faida. Wanajua Ile kodi waliwapa wakuu gani serkalini.Tunachohitaji watulipe kodi yetu kamili na wawadai wakuu waliowapa hayo mapesa ili wawafunge midomo!
 
- Yakwepa kulipa kodi zaidi ya Tsh Billioni 89
- Yaichezea serikali kwa miaka minne ikisingizia kuwa inapata hasara, kumbe ulikuwa ni mchezo mchafu, iliingiza faida ya zaidi ya Tshs Trillioni 1.79 za Kitanzania
- TRA yawabana watupe chetu.

=============================

barrick.jpg

Baraza la Rufaa za Kodi (TRAT), limeibana Kampuni ya Madini ya African Barrick Gold Plc (kwa sasa Acacia) baada ya kuridhika kuwa ilijenga mazingira ya kukwepa kodi ya Dola za Marekani 41,250,426 (Sh89 bilioni) kwa kipindi cha miaka minne mfululizo.

Fedha hizo zilizopaswa kulipwa na ABG kwa Mamlaka ya Mapato Tanzania (TRA) kama kodi ya zuio katika kipindi hicho, lakini ikakata rufaa kupinga kodi hiyo na baraza hilo kuipa haki TRA.

Katika uamuzi huo uliotolewa Machi 31, mwaka huu na Mwenyekiti wa TRAT, Jaji Dk Fauz Twaib, baraza hilo limekubaliana na hukumu ya Baraza la Rufaa za Kodi nchini (TRAB) na hoja za TRA kuwa ABG imekuwa ikifanya mchezo wa kukwepa kodi.

Kwa mujibu wa hukumu hiyo, ABG ilikwepa kulipa kodi hiyo kuanzia 2010 hadi 2013 kwa namna mbili, kwanza ikiwa ni kudai kuwa kampuni tatu zilizo chini yake zinazojishughulisha na uchimbaji wa madini nchini zimekuwa zikipata hasara.

Kampuni hizo ni Bulyanhulu Gold Mining Ltd, inayomiliki mgodi wa Bulyanhulu, North Mara Mining Ltd na Pangea Minerals Ltd, inayomiliki migodi ya Buzwagi na Tulawaka.

Hata hivyo, wakati kampuni hizo zikidai kuwa zilikuwa zikipata hasara, baadaye ilibainika kuwa kampuni mama ya ABG PLC, yenye makao yake makuu jijini London, Uingereza katika vipindi hivyo, ilikuwa ikitangaza kutoa gawio kwa wanahisa wake.

Gawio hilo lilitokana na mapato yaliyopatikana kutoka na shughuli zake nchini za uchimbaji madini, ambayo katika kipindi hicho cha miaka minne yalifikia Dola 818,431,285 za Marekani (Sh1.79 Trillioni).

Wakati wa usikilizwaji wa rufaa hiyo katika ngazi ya Bodi, TRA iliwasilisha taarifa ambazo zilitolewa na ABG za mapato za kila mwaka kama kielelezo ambazo ilidai kuzipata katika upelelezi wake.

Taarifa hizo ambazo ni moja ya vigezo vilivyojenga msingi wa uamuzi wa TRAB na TRAT, zinaonyesha kuwa 2010, ABG ilitoa gawio kwa wanahisa wake la Dola 259,542,367 za Marekani.

Katika kiwango hicho, TRA ilionyesha kuwa ilitakiwa kulipwa kodi ya zuio la asimilia 10 ambayo ni Dola 25,954,237 za Marekani, wakati kwa mwaka 2011 ABG ilitoa gawio la Dola 28,295,899 na kodi ya zuio kwa TRA Dola 2,829,5809.

Mwaka 2012, gawio lilikuwa ni Dola 70,124,620 wakati kodi ya zuio ni Dola 7,012,462 na mwaka 2013, gawio lilikuwa Dola 54,541,371, ambapo kodi ya zuio ilikuwa Dola 5,454,137 za Marekani.

Katika hukumu yake, TRAT imeelezea kushangazwa na mwenendo wa AGB na kampuni zake zinazoendesha biashara ya uchimbaji madini kutangaza kupata hasara katika kipindi hicho wakati kampuni mama ambayo pato lake linatokana na shughuli za kampuni hizo, ikitangaza na kutoa gawio kwa wanahisa wake.

Baraza hilo linaeleza katika hukumu hiyo kuwa TRAB katika kesi ya msingi, ilibaini katika ukurasa wa 123 wa taarifa yake (ya fedha), AGB inaeleza kwamba pato lake lote linatokana na shughuli za madini zinazoendeshwa na kampuni zake ndogo nchini.

Linaendelea kueleza baraza hilo kuwa taarifa hiyo ya AGB haionyeshi mbali na migodi ya Tanzania, hakuna shughuli nyingine yoyote duniani kote inayoendeshwa na ABG ambayo huchangia pato hilo.

Baraza hilo lilisema kitendo cha kampuni zake zote ambazo ndizo chanzo cha mapato yake zikitangaza kupata hasara, kinamaanisha kuwa hakuna gawio la kulipa kwa wanahisa wake na hazijalipa kodi ya kampuni zake kwa miaka yote hiyo.

“Kwa kweli tunaungana na Bodi (TRAB) kushangaa, kwamba hili linawezekana vipi. Ni jambo lisiloshawishi kwamba mrufani (ABG) aliweza kulipa gawio hilo wakati raslimali zake pekee ni kampuni tatu zinazopata hasara zilizoko Tanzania, ambazo hazipati faida kabisa na hazitoi gawio,” ilisema TRAT.

“Katika mazingira hayo ni sawa kuhitimisha hoja ya mjibu rufaa (Kamishna Mkuu wa TRA kupitia kwa Wakili wake, Noah Tito) kuwa miamala hiyo ni namna iliyotengenezwa na mrufani (ABG) kwa lengo la kukwepa kodi ilithibitika,” iliongeza TRAT katika uamuzi huo.

TRA baada ya kupitia vifungu mbalimbali vya sheria na hoja za pande zote, pia ilikubaliana na hoja za mamlaka hiyo pamoja na msimamo wa TRAB kwamba mrufani huyo ni kampuni mkazi nchini, hivyo anastahili kulipa kodi zote.

Source: Mwananchi

My Take:
Utawala wa JK umetuharibia sana hii nchi aiseee
Na mkurugenzi mkuu wakati huo alikuwa mtanzania mwenzetu,na kasomeshwa na serikali ya Tanzania buure lakini sasa ndio fadhila zake kwa Watanzania
 
ok, sina details , hila inawezekana hiyo kesi ilianza katika utawala wa mkwere, kuna process kama tatu kama sijakosea hiyo hapo ndiyo final stage, ss kwa kuwa kesi za bongo uchukua muda mrefu, ndio maana nikawa na wasi wasi huo, Pia nafikiri kuna room ya kwenda court of appeals
Well, sina details hivyo kwa hilo siwezi ku argue.
 
Bado sijaelewa, corporate tax inalipwa wakati gani? Kwa nini serikali haikufanya uhakiki wa kimahesabu kila mwisho wa mwaka kujua nini wameingiza, matumizi, faida/hasara ili wajihakikishie uhalali wa hasara/faida kampuni inayopata? Serikali inaweza kuingilia mahesabu ya shirika/kampuni yoyote, una maana gani ukisema sio rahisi kupata hayo mahesabu?
Nielimishe...

Mahesabu yanafanyika kila mwisho wa mwaka, ila kuna vitu vingi hawa jamaa walikuwa wanaongopa au kutoa data tofauti, na vitu hivyo vilikuwa havijagundulika serikalini, na kumbuka wakati tunaingia huko, tulikuwa hatujavihusisha baadhi ya vitu, ila kwa sasa wataalamu wetu, wana weledi wa kutosha, na sasa vinahusishwa katika mahesabu. Na vingi walivyokuwa wanaongopa, ni vifaa vya uzalishaji, vingi walikuwa wanatoa data ambazo si kweli.
 
Back
Top Bottom