BigTall
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 497
- 1,200
Kuna wakati najiuliza kwani magari yameongezeka katika Barabarara hiyo maarufu kwa jina la Morogoro Road? Utaratibu wa uongozaji magari ni mbovu au ni nini hasa ambacho kimetokea?
Askari wa Usalama wa Barabarani wanatakiwa kuangalia namna ya kufanya, haiwezekani barabra ina lami, kuna mwendokasi lakini bado foleni imekuwa ni kero.
Askari aache ku focus kuvizia watu ili wawapige “mabao” badala yake waangalie jinsi ya kutafuta utatuzi, kwani foleni inasababisha watu wengine kuchepuke pembeni na wakifanya hivyo ndivyo hali inavyozidi kuwa mbaya.
Shughuli za uchumi zinasimama, mambo hayaendi kutokana na foleni hiyo ya kila asubuhi.