Barabara ya kituo cha Masiliano kinatia aibu!

FRANCIS DA DON

JF-Expert Member
Sep 4, 2013
37,890
43,782
Kituo cha Mawasiliano kilichochukua nafasi ya kituo cha ubungo ni moja ya vituo bora kabisa vya daladala afrika mashariki na kati. Lakini cha kushangaza na kutia aibu ni kwamba barabara inayoiunganisha barabara ya Sam Nujoma na kituo hicho iko katika hali mbaya ya mashimo mashimo kama mahandaki, ina vumbi kama kiwanda cha cement na wakati wa mvua ni mabwawa na matope kwa kwenda mbele. Urefu wa hii barabara ukiunganisha na kile kipande kinachoenda hadi Sinza ni chini ya 1km. Sasa je, ni nini hasa kinachosababisha miaka yote hii kipande hiki kisiwekwe lami..?!

=======================================
UPDATE: (20/03/2017) Baada ya kuleta malalamiko hapa jf takriban wiki moja iliyopita, leo mkuu wa mkoa wa Dar mh.Paul Makonda, katika sherehe za uwekaji jiwe la msingi la ujenzi wa ubungo flyover, amesema bajeti kwa ajili ya barabara ya kituo cha mawasiliano imeshatengwa na ujenzi utaanza muda wowote kuanzia sasa. Kweli jf inamkono mrefu.
 
Natarajia ujenzi utaanza hii karibuni maana ni mandhari chafu sana kwa kituo kizuri kama hiki, napita hapa muda huu, ni aibu!
 
Afrika mashariki na kati!!

Anyway lazima iwepo bajeti kwa hizo barabara na ilitakiwa bajeti itengwe tangu siku ya kwanza wanapanga kujenga kituo hicho
 
Afrika mashariki na kati!!

Anyway lazima iwepo bajeti kwa hizo barabara na ilitakiwa bajeti itengwe tangu siku ya kwanza wanapanga kujenga kituo hicho
Pesa ipo, watueleze tu kuna sababu zipi za msingi zinazopelekea miaka yote hii kuacha ile aibu pale!
 
daah mtoa mada kula tano mkuu. ile road ni mbovu hakuna mfano yaan haiendani na ubora wa kituo cha mawasiliano. nashangaa manispaa ya kinondoni wanashindwa nini kujenga ile barabara ambayo haifiki hata km 1 kwa lami ni aibu kwakweli. daladala zinaharibika mno kwa njia ile mbovu tena ubovu huongezeka kipindi kama hiki cha mvua. manispaa waone aibu. mkuu wa mkoa naye kaomba msaada china wajenge uwanja wa mpira wa bandari kwa millioni 400 kashindwa kuomba msaada wa lami kwenye road isiyofika hata km 1.
 
Mkuu tuwekeee picha tuone kwa sasa, maana wengine atupiti huko tuna muda mrefu, ndio maana hata serikali aijaifatilia weka mipicha tena ya madimbwi kabisa, ili picha zikijaaa umu, waandishi wa habari watafanyia kazi kuweka katika Media zao na mwisho Mkulu ataona
 
Ujinga mwingine ni kulazimisha gari zinazotokea mbezi kuelekea Makumbusho kuingia ndani ya kituo cha mawasiliano..!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…