Mohamed Said
JF-Expert Member
- Nov 2, 2008
- 21,794
- 31,804
TBC1 BAKARI MSUYA NA TBC TAIFA DAVID MAYUNGA WAMEPIGA HODI MAKTABA: KIPINDI CHA MUUNGANO
Sikutegemea kuwa nitatembelewa kwa siku moja na vijana hawa watangazaji hodari kutoka TBC 1 Bakari a Msuya na TBC Taifa David Mayunga kunihoji kuhusu Muungano wa Tanganyika na Zanzibar mwaka 1964.
Sikutegemea kuwaona vijana hawa wachangamfu wakipishana kwenye kizingiti cha mlango wangu huyu anabisha hodi anaingia yule anaaga anatoka.
Kitu kimoja kilinifurahisha sana ni kuwa hofu yangu ilikuwa kwa kuwa wote wanatoka chombo kimoja cha habari TBC mahojiano yetu yatafanana kwa hiyo kuondoa ladha kwa mhojiwa na halikadhalika watazamaji na wasikilizaji.
Haikuwa hivyo.
Haikuwa hivyo ila kwa swali moja tu.
Huenda kwa kuwa mimi ni mzee na wenzangu ni vijana wadogo sana wote walitaka nieleze nchi mbili hizi zilikuwaje kabla ya Muungano.
Wote wanasema hawakuwapo wakati wa Muungano.
Wote walitaka nieleze nini kifanyike kizazi cha sasa kiwe na uzalendo mkubwa na kuthamini Muungano.
Niliwapitisha kwa haraka na wima wima kwenye historia ya Mapinduzi ya Zanzibar ya mwaka 1964.
Baada ya hapo ndipo nilipowakalisha kitako tuzungumze kuhusu Muungano.
Vipindi hivi In Shaa Allah vitarushwa leo Ijumaa tarehe 26 Aprili siku ya kusheherekea Muungano.
Picha ya kwanza Bakari Msuya na picha ya pili ni David Mayunga.