Baadhi ya maamuzi yananayotolewa mamlaka za maamuzi yanaumiza wananchi

Danken Mbombo

JF-Expert Member
May 30, 2015
651
339
Mamlaka zinazohusika kutoa maamuzi ziwe makini kwani baadhi ya maamuzi yao hayana tija yoyote kwa wananchi bali yanawaumiza tu.

Mfano 1: Barabara ya Uhuru, toka mnazi mmoja hakuna kituo cha dala-dala hadi Karume. Abiria toka kariakoo analazimika kutembea umbali mrefu au kulazimisha daladala zisimame kupakia popote wakati traffic wanakodoa mimacho

Mfano 2: Barabara ya Mandela, abiria wanaokuja Ubungo (bus terminal) wakitokea Buguruni, Tabata n.k wanashushwa kituo cha Riverside, ambapo ni zaidi ya kilometa mbili hadi bus terminal, wanalazimika kutembea na mabegi kichwani, hii ni adha kubwa sana.
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…