Baada ya Muungano: Mwinyi ndio Rais pekee aliekuwa mstaarabu, mstahamilivu na hekima

Kwa hiyo unapomlinganisha Raisi Magufuli na Mwinyi, unachotuambia ni kwamba ni bora Tanzania iwe na raisi asiyejali kitu kuliko yule anachukia kuachia mambo ovyo ovyo tu.
Siwezi kumlinganisha Rais Mwinyi na yeyote lakini ukweli utaendelea kuheshimiwa kuwa alikuwa bora kuliko wote. Leo tupo hapa kutokana na busara zake. Moja ya hekima na busara zake na anavyojua kucheza na lugha pale aliposema " Alioyafanya Rais JPM ndani ya kipindi cha Mwaka mmoja tu ni mengi na makubwa kuliko yaliofanywa na sisi viongoza tuliomtangulia kwa pamoja." ( mpangilio ni wangu)

Hapana unakosea sana. Alichofanya Mwinyi ambacho wewe unatafsiri kuwa demokraia ni kwamba aliachia nchi ijiendeshe yenyewe bila kufanya lolote, na kila mtu akafanya kile alichotaka bila bugudha yeyote toka serikalini - ruksa. Kila kitu kibaya ambacho unaweza kuwazia Mwinyi aliachia bila kuchukua hatua yeyote, ndio maana unaona kama Mwinyi alikuwa bora kwa sababu hakubana uhuru wa watu katika mambo yote.
Hapana sikosea hata kidogo isipokuwa wewe ni mkosefu wa fadhila usiokuwa na hata hata ya kuvaa nguo. Sielewi umri wako lakini wale walioishi utawala wa awamu ya kwanza hawezi kuthubutu kuzungumza unayoyanena . Mwinyi Alipochukua uongozi
1. Tanzania imekuwa imefilisika kabisa kama taifa
2. Utawala uliotangulia ulilazimisha kila raia awe masikini wa kutupwa , mbali yakulazimisha raia kufunga mkanda hata viduka vya vijiji vinavyouzwa maharage na viberiti vilipigwa marufuku katika opresheni maalum " funga Mduka
3. Taifa lilikabiliwa na njaa kiasi cha kuomba chkula kwa wahisani adui . Watanzania walilazimishwa kula sembe la kijani, maarufu " sembe la Yanga" huku mikebe iliofungiwa kukiwa neno kubwa " unfit far human consumption"
4 watu wanakwenda nusu uchi, hawakogi wala kufua. Sabuni, dawa za meno nk. zikiitwa " luxury"
Anapochukua uongozi katika hali kama hiyo na ukaimudu hapo ndipo unapoweza kumpima Rais bora, sio waliokuta uchumi imara na kuuvuruga.
Rais Mwinyi mbali alikuwa ni mtu wa busara alikuwa sio tu kukemea maovu lakini ni mchukivu wa maovu na alionyesha mfano huo pale Tabia za kuuana ovyovyo aambazo mpaka leo zinaendele ukukitoa kipindi chake, alijiuzulu kubeba jukumu.

Mwinyi alisema yeye ni kichuguu na Mwalimu ni sawa na mlima Kilimanjaro!
Kasome tena kiswahili cha watu wa pwani. Hilo ni tusi la kistaaarabu.
Umewahi kukutana na watoto matineja wakakuambia sie baba yetu sio noma bali ni mshikaji sana - basi ndio alivyokuwa Mwinyi. Hiyo sio demokrasia, ni kuwa "laissez-faire" - mtu asiyejali mambo (attitude of letting things take their own course, without interfering)
Sijui tafsiri sahihi ya demokrasia lakini ilikuwa hivyo na uchumi ukawa bora kihalisia na sio kwa takwimu, watu wakaweza hata kupiga mswaki na kuoga, kula unachokitaka na kukipenda. kutoa maoni bila kusakamwa, kuandamana bila kudhibitiwa kwa maji washwasha, kuruhusu mikusanyiko na kubadilishana mawazondio unayoita "laissez-faire" basi mimi natamani ingeendelea
Matokeo yakawa kwamba jamii ya Kiasia nchini ikawa na nguvu sana,
Hii ndio sura yako kamili ya kibaguzi na choyo.Miaka mingapi tokea Mwinyi amalize uongozi wake, uchumu wa Tanzania umo mikononi mwa nani? na tokea lini uchumi wa Tanzania uliwahi kuwa mikononi mwa wasukuma?Akina Rajpar tena wakati wa Nyerere alikuwa ana nguvu kuliko serikali na hapo ilipotaka kumjaribu kumdhibiti alihama na gereza lote la ukonga!
Na kama Mrema alivyowahi kusema, kama Mwinyi aliweza kuwa raisi wa nchi hii kwa miaka kumi, basi kila Mtanzania anaweza kuwa raisi wa Tanzania
Hivi mrema ni nani Tanzania. Huoni hata aibu kumnukuu. Kama M rema anaweza kuongoza taasisi kwa zaidi ya miaka 20 basi hata hayawani anaweza.
Ukweli ni kwamba hakuna kipindi cha uongozi mbovu Tanzania imewahi kupitia kama kipindi cha Mwinyi. Huo ndio ukweli, upende usipende.
Huo ni ukweli, upende usipende. Hata hili lakuweza kumsema katika Baraza hili la JF ni matunda ya Mzee Ruksa kuhusu vyombo vya habari.
 
Back
Top Bottom