Baada ya kumdhibiti Makonda, nisisikie mtu akilalamika juu ya madawa ya kulevya!

Mkuu acha tu kungekuwa na uwezekano D Trump akatutupia Makombora ya nyuklia watanzania wote tukatoweka kwenye uso wa dunia sisi ni wanafiki sana ni wajuaji wa vitu hata tusivyokuwa na ujuzi navyo
mmmh! hapana aisee mie nataka kuishi Kingsharon
 
Inaonekana kuna watu wamejipanga kisawasawa kumdhibiti Makonda kwenye hii vita ya madawa.

Sikutegemea kuona baadhi ya Watanzania kumkashifu Makonda kwamba anatafuta sifa! Sifa jwa ajili ya nini? Sikutegemea kuona baadhi ya wabunge kusimama na kuanza kumpinga Makonda.

Sasa kinachofuata, Makonda ataachana na hii operesheni na hapo madawa yatakuwa yameruhusiwa rasmi hapa nchini.

Na kwakuwa tumeshindwa kumasapoti Makonda kwa sababu ya mahaba yetu ya kisiasa, nisisikie mtu akilalamika kuhusu madawa ya kulevya tena.
Na wewe acha akili za kitoto. Hivi unamsifia Makonda kwa lipi hasa? Mtu ambaye ameshindwa kukamata hata nusu kilo ya madawa amekalia kutaja majina ya kushuku ndio unamwita mpambanaji? Bora akae kimya tu.
Vipo vyombo mahsusi (Polisi & Tume) kwa kazi hiyo
 
Ukimya wa waziri wa mambo ya ndani unatia shaka mno, ukitaka kujua biashara hii kuwa wanaohusika zaidi ni wenyewe watunga Sheria washika madaraka angalia nguvu inayotumika kuanzia bungeni mpaka mitaani kumdhibiti makonda,
Nachoweza kusema ikiwa makonda kweli umeamua kupambana tena bila chuki au umetumwa tu kuwatafuta watu fulani basi mungu awe nawe na ufanikiwe na ikiwa kinyume chake uangamie kabisa
Wazili wa mambo ya ndani bora alivyoamua kunyamaza kimya,
maana huwezi kudandia gari ambalo hujui linaelekea wapi na Kituo chake cha kwanza wapi?
 
Na wewe acha akili za kitoto. Hivi unamsifia Makonda kwa lipi hasa? Mtu ambaye ameshindwa kukamata hata nusu kilo ya madawa amekalia kutaja majina ya kushuku ndio unamwita mpambanaji? Bora akae kimya tu.
Vipo vyombo mahsusi (Polisi & Tume) kwa kazi hiyo
WaTz tunapenda sana MAJUNGU. Mtu akiwa bingwa wa majungu huyo kwetu ndiye shujaa. Ukisoma maoni yanayounga mkono haya majungu ya Makonda, unabakia mdomo wazi. Kinachoshangaza hata yule Kamanda aliyepigiwa majungu mbele ya PM kwamba alipokea rushwa ya milioni 5 kutoka kwa wauza shisha, naye bila kupepesa macho yupo mstari wa mbele kutekeleza majungu ya Makonda! Hata slogan ya 'hapa kazi tu' imepotea mwelekeo kutokana kutawaliwa na majungu - nitumbue, sisitumbue? Tumbua babaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaaa! Watawala hawataki kuzingatia sheria na kanuni zilizopo (hata kama ni mbovu), na wananchi wanashangilia kuona sheria zinavunjwa na watawala. Hiki ni kipindi cha mvurugano na mtafaruku.
 
Inaonekana kuna watu wamejipanga kisawasawa kumdhibiti Makonda kwenye hii vita ya madawa.

Sikutegemea kuona baadhi ya Watanzania kumkashifu Makonda kwamba anatafuta sifa! Sifa jwa ajili ya nini? Sikutegemea kuona baadhi ya wabunge kusimama na kuanza kumpinga Makonda.

Sasa kinachofuata, Makonda ataachana na hii operesheni na hapo madawa yatakuwa yameruhusiwa rasmi hapa nchini.

Na kwakuwa tumeshindwa kumasapoti Makonda kwa sababu ya mahaba yetu ya kisiasa, nisisikie mtu akilalamika kuhusu madawa ya kulevya tena.
Mkuu pole sana kwa kupagawa mpaka unaandika matusi,
Lakini je uliwahi ona wapi muhalifu anatangaziwa kwamba tunakutafuta kwa wizi tena siku tarehe na saa ya kukamatwa anapewa? Hapo hata kama Mali alikwiba ziko nyumbani kwake atazihamishia sehemu nyingine,je hiyo nayo utaiita vita?
 
Wanaompinga Makonda mmelaaniwa.Natamani siku niwaone watoto wao nao wamekonda mpaka mafuvu ya kichwa kama Chid Benzi ndio wajue madhara ya madawa ya kulevya.
 
Yes!!!!
Mh. Makonda ni Mw/kiti kamati ya usalama kwa Dar tu.
Usalama wa watu wa Dar es salaam unamuhusu Makonda kwa asilimia zote.
 
Vipi kama waliotajwa wamo kwenye hiyo listi na ndio wameanza kushughulikiwa kwa kuitwa kuhojiwa
Kwa hiyo kama orodha ndio ile unadhani kwa nini imeandikwa na mtu kama anaekimbia kulowana na mvua.maana majina yanakosewa,zimetumika aka bila majina halisi na mengine jina mojamoja.
 
hii ni kama muvi na makonda alijua kuwa kwa kutokufuata utaratibu lazima atapingwa kisha ataachana na hiyo kitu lakini kama angenitumia mimi eddy_mhando niende kwa hao aliowatuhumu kuhusika na uuzaji kisha serikali ikatoa fedha nikaenda kununua...kisha nikakamatwa mimi na huyo muuzaji nadhani makonda angekuwa amefanya kazi kubwa sana inayohitaji pongezi...lakini kwa kuwasingizia watu inafaa kumuita MPUMBAVU anaye wasingizia wengine
 
Wanaompinga Makonda mmelaaniwa.Natamani siku niwaone watoto wao nao wamekonda mpaka mafuvu ya kichwa kama Chid Benzi ndio wajue madhara ya madawa ya kulevya.
Kila MTU anachukia dawa za kulevya makonda angetumia njia stahiki hata mm nungewataja wa mtaani kwetu njia anayotumia sii sahihi tatizo anapenda kujionesha na kuongea huko kwenye TV hana nia yoyote wala mipango mkakati...
Shkamoo sugu..... Aka wa mitulinga
Akikaa kimya ataenda kumweleza nini Mungu?
 
Hakuna anayepinga vita dhidi ya madawa ya kulevya kinachopingwa ni taratibu alizotumia busara, sheria , katiba na haki vifuatwe!
 
Madawa ninin mbona wanaokufa ukimw hamuwasemi kwan sio watu? Nabado hamjatokomeza kuudhibit ukimw... Vipo ving vinaua watu alaf mpo alaf leo et madawa... Kwan kunamtu kazaliwa kichaa hapa? Achen upuuz kila mtu analife Lake anafanya kile kinachomnufaisha naanaona kina faa.... Mung alitupa akil ukizitumia ovyo kimpango wako!!!!!
 
Huyu jamaa angedhamiria vita hii angewaunga mkono vyombo husika kufanya uchunguzi na kuwashikilia wahusika kabla ya kuwatangaza bila ushahidi. Vyenginevyo anafaya usanii tu na kuharibu ushahidi wowote kama upo. Aache kuchafua majina ya watu kwa kukurupuka.
 
makonda sio polisi wala sio waziri wa mambo ya ndani wala sio mkuu wa kitengo cha kupambana na madawa ya kulevya so kaingilia kazi za watu awe mpole,aanze kujitaja yeye kwani nae katajwa kuwa anahusika,
makonda anafanya kwa eneo lake la mkoa kwa kamati ya ulinzi na usalama sawa na kamatakamata ya gongo na mihadalati mawilayani ambayo ipo kila siku....waziri husika atafanya kama shuguli ya kitaifa, ila hamzuii Makonda kufanya kwa eneo lake.
 
Back
Top Bottom