Azam Tv wamelewa sifa

Tyupa

JF-Expert Member
Aug 11, 2013
802
657
Matangazo ya mpira wa ligi kuu Tanzania bara na yale ya nchi jirani yameanza kuwa na dosari. Kwa mtu mgeni anaefungua tv kuangalia matangazo hayo hataelewa kama matangazo hayo ni LIVE au RECORDED kwa sababu hayo maandishi siku hizi hayawekwi.

Hata matangazo ya ligi za nje kama Ulaya pia alama hizi haziwekwe.Hatujui sababu ya kuondoa maandishi hayo ni nini lakini AZAM tv wanapaswa watuiambie. Tatizo lingine ni lile liloonekana katika mechi ya Yanga na Mtibwa tarehe ya jana 5/02/2017 katika uwanja wa Jamhuri Morogoro.

Kamera za Azam tv zilitegwa nyuma ya bendera ya taifa iliokuwa inapepea uwanjani hapo. Matokeo yake badala ya kuangalia mpira vizuri bendera hiyo ulikuwa inafunika screen karibu theluthi moja na kufanya matangazo kuonyesha bendera badala ya mpira.

Kazi ya fundi mitambo aliekwepo pale inashangaza ni kwa nini hakuona kuwa kamera za Azam zinazibwa na hiyo bendera. Uongozi wa Azam unapaswa kuwa makini na wafanyakazi waliopewa majukumu ya kuwezesha chombo hiki kinachopendwa na wengi. Ni matumaini yetu kuwa kasoro hizi mbili zinarekebishwa haraka.
 
Ni kweli,,,hiyo LA live walishasema lipo nje ya uwezo wao mkuu ila ni kwa upande Wa mechi zinazochezwa tz tu,,,kuhusu LA mechi za nje kwa kweli neno live linakuwepo,,,pia Jana mechi ya mtibwa waliomba radhi kwamba hakukuwa na namna nyingine zaidi ya kuitega kamera pale,,
 
Hayo maandishi mawili tu au moja kwa sababu hayawezi kuwekwa yote kwa wakati mmoja yana gharama gani? Ukisikia duniani kuna maajabu haya nayo ni mojawapo.Hivi kweli utajiri wote wa Azam wanashindwaje kugharamia neno moja lenye herufi nne tu la LIVE au RECORDED?
 
Mkuu hawana mamlaka ya kuweka hilo neno live kwenye Vpl,,,,ila LA liga wanaweka maana wana haki hiyo,, nadhani umenielewa,,nisitumie nguvu kubwa maana hata elimu yako nina wasiwasi nayo maana nimekuelewesha mwanzo vizuri huelew
 
Mkuu hawana mamlaka ya kuweka hilo neno live kwenye Vpl,,,,ila LA liga wanaweka maana wana haki hiyo,, nadhani umenielewa,,nisitumie nguvu kubwa maana hata elimu yako nina wasiwasi nayo maana nimekuelewesha mwanzo vizuri huelew
Wewe unaongea kama nani kwa dharau kiasi hicho? Kumbuka kwamba kama wewe una elimu juu ya jambo fulani haimanishi kwamba na wengine wote wanayo hiyo elimu.Wewe utakuwa nayo na wengine watakuwa na ujuzi mwingine. Kwenye matangazo ya mpira kuna majina ya timu huandikwa kwa mfano Simba vs Yanga.Lakini sasa ugumu unatoka wapi kuandika tu neno mmoja 'LIVE'.Hayo mamlaka wanayokataza kuandika neno hilo ni mamlaka gani na wanakataza kwa sababu gani.Je,hilo neno liko kama kirusi na likiandikwa tu TV yote ya Azam inaungua!!!.Wewe si mfanyakazi wa Azam na ndio maana majibu yako ni utumbo mtupu na ikiwa ni mfanyakazi wa Azam basi wewe ni mmojawapo waliolewa sifa.
 
Bendera haiwezi tolewa kwenye viwanja vya watu Jengeni vyenu visivyo na Bendera.

Samata katupia Moja Kombe la Ulaya Wanaongoza Nne dhidi ya Moja
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…