Waufukweni
JF-Expert Member
- May 16, 2024
- 1,093
- 2,620
Leo nikiwa namsikiliza Aunt Sadaka, Mwanasaikolojia na Mshauri wa masuala ya Malezi, Ndoa na Mahusiano kwenye redio, nikajikuta nakumbuka mambo ya utotoni na vile vipondo. Aliweza kuzungumza kwa kina kuhusu jinsi wazazi au walezi wanavyopaswa kuwaachia watoto wao nafasi ya kujifunza kupitia majaribio yao wenyewe.
Alisema: "Tangu mtoto anapokuwa mdogo muache apande juu ya dirisha. Muache athubutu. Kuna kile kipindi cha 'Naweza' au 'Siwezi'. Hiyo ni miaka Mitatu hadi Sita. Kile kipindi cha mbio ndio kipindi ambacho mtoto anatakiwa ajaribu kupanda miti, ateremke. Achore friji ndio kipindi ambacho kinamfanya mtoto ajiamini kwamba ana uwezo.
Aunt Sadaka aliendelea kusema kwamba, "Mtoto akifika umri wa miaka 11, tayari atakuwa anajua anachoweza na asichoweza. Wazazi wanapaswa kuwa tayari kumwachia mtoto nafasi ya kuingia kwenye changamoto, mradi tu hazimletei matatizo makubwa."
Maneno yake yalinikumbusha jinsi michezo ya utotoni ilivyokuwa na nafasi muhimu kwenye kujenga ujasiri na uwezo wetu wa kukabiliana na dunia!
Hili unalionaje mdau?
Credit: PB/Clouds Fm
Soma==>Nguvu za kumfanya mtoto wako awe mtu bora zipo kwako