Askofu Gwajima amempongeza Rais Magufuli kwa kumtumbua Prof. Muhongo na kusema liwe ni funzo kwa wale wanaodhani nafasi zao katika madaraka zitakuwa niza milele.
Gwajima amesema, ''Muhongo amekomeshwa vizuri sana kwa sababu wakati ule watu wananunua vitalu vya gesi na wazawa wa Tanzania wakataka wanunue yeye anawaambia hela zenu niza kufungia maandazi''.
Gwajima alienda mbali zaidi na kusema, ''Maandazi yamemfunga yeye badala ya watanzania aliokuwa anawaambia wana pesa za kufungia maandazi''.
Gwajima amemuomba Rais Magufuli asilegeze kamba kuhusiana na suala la maliasili za taifa.
Alisema, ''Namuombea Rais akaze hapohapo, yaani itabidi niombe maombi maalum ili roho yake iwe ngumu akaze hapohapo, hayaendi makontena pamoja na kwamba kuna baadhi ya watu wanapiga kelele eti atashitakiwa''.
''Eee mtashitakiwa, hayaendi makontena, eee mtapelekwa arbitration, hayaendi hayaendi makontena mpaka mzungu atoe macho awe mwekundu kabisa, hayaendi makontena''. Alisema.
Aliendelea kusema, ''Huu sio wakati wa kupiga porojo na kuanza kum-criticize Rais na kusema unajua Rais ameamua vibaya, angefuata process''.
Gwajima alienda mbali zaidi na kusema, ''Yaani wanataka Rais afuate process huku madini yetu yakiendelea kuondoka, ningekuwa mimi ni Rais ningefanya zaidi ya alichokifanya Rais''.
Kwa alichokisema Gwajima angalia video: