chiembe
JF-Expert Member
- May 16, 2015
- 15,163
- 25,910
Askofu Malasusa anakamata usukani wa kuongoza KKKT tarehe 21/1/2024. Askofu Benson Bagonza ameeleza kwamba kanisa hilo linegubikwa na madeni ya kutisha yanayotokana na ubadhirifu uliokithiri wakati wa uongozi wa Dk. Shoo.
Bagonza ameeleza kwamba Kanisa hilo limekosa uhalali wa kukemea ubadhirifu na mahala pengine kwa kuwa ndani ya kanisa kumeoza.
Kauli hii ya Bagonza inanifikirisha sana, gasa ukizingatia Dk. Shoo, mshirika mkubwa wa chadema, alikuwa mstari wa mbele kushambulia kila mtu, ikiwemo serikali kwamba haizingatii utawala bora.
Kumbe wakati akifanya mashambulizi hayo, nyumbani kwake palikuwa pamevunda. Haijulikani hao chadema anaowaongoza kiroho kama wana nafuu.
Askofu Bagonza aliendelea kueleza kwamba, wakati wa uongozi wa Dk. Shoo, kwa mara ya kwanza katika historia, mali za kanisa zilipigwa mnada kufidia madeni ya kifisadi.
Hivi karibuni, seminari moja ya morogoro ililazimika kuuza mali zake ili kulipa wafanyakazi, na bado deni halikuisha. Na Hospitali moja ya kanisa iliyo kanda ya kaskazini ineripotiwa kuwa hoi. Pia hotel moja huko mikoa ya nyanda za juu kusini inayomulikiwa na kanisa iliripotiwa kudaiwa mabilioni, ambayo hayajulikani yalipo mpaka sasa.