nizakale
JF-Expert Member
- Oct 23, 2019
- 4,021
- 2,932
Traffic wilaya ya Sengerema wanatakiwa wazinagatie taratibu za kazi zao badala ya kuwakomoa hasa wenye private cars.
Siku moja nilisafiri kuelekea Geita kupitia Busisi. Nimevuka kivuko salama na nikaanza safari yangu kuelekea Geita.
Kote nilikopita nilizingatia alama zote za barabarani, huku wenye mabasi wakipita mwendo kasi hata kwenye sehemu ambazo kuna alama ya 50 Kph. Nilipofika Sengerema mjini huku nikiwa na mwendo wa 40 kph baada tu ya kupita round about mbele kidogo, traffic mmoja akanisimamisha. Niliposimama akaomba leseni yangu.
Nikampa baadaye akanionyesha picha ya gari inayofanana na yangu eti huko nyuma nimeenda mwendo kasi kwenye alama za pundamilia, nikamuuliza ni wapi hapo akasema hajui. Nikamhoji hiyo picha namba ya gari ni ngapi, hana jibu. Nikamuuliza tena ni magari mangapi yanayofanana na yangu yamepita njia hii, hakuwa na jibu.
Akaniandikia faini na kunipa control namba. Kweli kitendo hicho kiliuma sana maana sikuwahi kwenda mwendo kasi. Mambo haya yamezidi sana wilaya hii. Sijui kwanini na hutaona bus likisimamishwa nadhani kuna namna ambayo huwa wanakubaliana na wenye mabus.
Mbona wilaya zingine hakuna uonevu kama huu? Uonevu kama huu iko siku utaleta maafa. Maana siwezi kuonewa hivi hivi ni bora niende kunyea debe. Upuuzi kama huu huwezi kuuona Nyamagana, Misungwi wala Geita.
Kama wilaya yenu ni maskini tafuteni vyanzo vingine vya mapato badala ya kuonea wenye private car. Bora wapige picha na plate namba ionekane siyo kulazimisha eti, ohh picha inafanana na gari yako.
Kweli inauma sana.