Anne Kilango Malecela anena haya baada ya taarifa ya kuenguliwa nafasi yake

Inasikitisha sana ,nadhani sio vizuri kukejeli au kushabikia swala hilo hivi ni mtumishi yupi wa umma ambaye hafanyi makosa? Wapo wana makosa makubwa kuliko hili labda wana bahati au zamu yao haijafika

Umesema jambo la maana sana. Siungi mkono uzembe wa shangazi huyu, lakini hili siyo jambo la kushabikia. Viongozi wengi wanadanganywa na watu wa chini yao, na wanapigwa majungu. Inawezekana hizi zilikuwa ni njama za kumwangusha au pengine yako mengi nyuma ya pazia. Ripoti za TISS zimefanya kazi.
 
Ila graph imeshuka kwa kazi mno...Mbunge<<, Waziri>>, Mkuu wa Mkoa>>, Mwanachama wa CCM>> raia!!!??? (Baada ya kufukuzwa uanachama).

Kwa nini awe raia?

Kwa katiba ya Chama cha Mapinduzi ya mwaka 2012 inaelezea masharti ya kuwa mwanachama(ukikiuka masharti siyo mwanachama). Mojawapo ya masharti hayo ni

....(6) Kuwa wakati wote ni mfano watabia nzuri kwa vitendo vyake nakauli yake, kuwa mwaminifu nakutokuwa mlevi au mzururaji.

Katiba ya CCM (2012) inasisitiza kuwa ...
13.(1)Uanachama wa mwanachamautakwisha kwa:-
.....................
..........
..........................
(e) Kutotimiza masharti ya uanachama

source: KATIBA YA CCM

Ufafanuzi wangu usiyo rasimi: "...Mama kakosa uaminifu, kauli yake ya kidanganyifu, hajawa mfano wa tabia nzuri...."
===============
My take: yangu nyingine kwa suala la wabunge kudai rushwa wakuu wa mikoa kutokuwa waaminifu wakati wanatokana na CCM si ni kukitega chama na kiongozi wake kweli.???
 
Watu wote alioteuliwa na chama atahakikisha anawang'oa kwa mtindo huu hadi awamalize wote. Ndio maana kila mtu anajiuliza January aliponaje? Kuna wengi tu alioteuliwa na chama chake ambao yeye hawataki hawatamaliza ungwe, ni wakati wa kusubiri tu na kuona.

Ova
 
Mkuu hizo habari hazitusadii vipi wakati ni kodi yetu ndio iliyokuwa ikikwapuliwa.....

Binafsi simjaji Mama Ane Kilango kama yeye, bali Ofisi ya Mkuu wa Mkoa ikiongozwa na yeye.

Hili la Mama Ane halina tofauti na ufisadi, au ufisadi nao ni mambo binafsi.

Mkuu tumia busara kidogo
ndani ya mwezi mmoja wewe ungeweza kutaja watumishi hewa?
haya mambo yako complicated.......sio ya kushangilia tu
 
Huyu mama ndio alikuwa nguzo kuu ya uchumi kwa familia ya Malecela, sema ndio hivyo tena, kisicho riziki, hakiliki!
Kwa hilo hapana bro Mussa! Malecela analipwa 80% ya Kassim Majaliwa hadi kufa kwake! Hizi daily operations hazina shida kwake yeye ni PM mstaafu? Tuache kakorosho hata kama huipendi familia au humpendo John Malecela! Tuache fitna hazina msingi
 
Leo taarifa ambayo metrend vya kutosha kwa muda mfupi, ni kuhusu Rais wa J.M wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mama Anne Kilango Malecela katika nafasi hiyo.

Mwanasiasa huyu Mkongwe amekumbwa na Panga hili baada ya kutoa taarifa hadharani kuwa, Mkoa wa Shinyanga haukuwa na watumishi hewa.

Kauli ambayo ilikinzana na tume rasmi ya uchunguzi iliyotumwa mkoani humo, ambapo iligundua watumishi hewa 45 na bado uchunguzi Zaidi unaendelea.

Akiongea na kituo cha radio cha Times Fm,Kilango amedai kuwa hana taarifa juu ya utenguzi wa nafasi hiyo kutoka kwa aliyemteua.

“Jamani Mimi sina taarifa sipendi kukizungumzia maana yake sijaambiwa na aliyeniteua, sina la kukwambia.” Alisema na kukata simu.

Anne Kilango Malecele amedumu kwenye nafasi hiyo kwa majuma kadhaa, hata mwezi mmoja hajafikisha.

Chanzo:
Swahilinews.co.tz
 
Kwao Same walimkataa kumrudishia ubunge, JPM akawaona wajinga akampa uRC na leo kavunja rekodi kwa kuwa mkuu wa mkoa wa kwanza tangu tujitawale kutimliwa kazi muda mfupi baada ya kuapishwa.
Serikali ya Magufuli oyeeee .....
Same oyeeeeeee ......!
Achana na Rutengwe ampe Kanali Fabian Massawe aone kazi inavyofanywa.
 
Leo taarifa ambayo metrend vya kutosha kwa muda mfupi, ni kuhusu Rais wa J.M wa Tanzania Dkt John Pombe Magufuli kutengua uteuzi wa aliyekuwa mkuu wa Mkoa wa Shinyanga Mama Anne Kilango Malecela katika nafasi hiyo.

Mwanasiasa huyu Mkongwe amekumbwa na Panga hili baada ya kutoa taarifa hadharani kuwa, Mkoa wa Shinyanga haukuwa na watumishi hewa.

Kauli ambayo ilikinzana na tume rasmi ya uchunguzi iliyotumwa mkoani humo, ambapo iligundua watumishi hewa 45 na bado uchunguzi Zaidi unaendelea.

Akiongea na kituo cha radio cha Times Fm,Kilango amedai kuwa hana taarifa juu ya utenguzi wa nafasi hiyo kutoka kwa aliyemteua.

“Jamani Mimi sina taarifa sipendi kukizungumzia maana yake sijaambiwa na aliyeniteua, sina la kukwambia.” Alisema na kukata simu.

Anne Kilango Malecele amedumu kwenye nafasi hiyo kwa majuma kadhaa, hata mwezi mmoja hajafikisha.

Chanzo:
Swahilinews.co.tz
Watu wa aisomba namba vibaya.... We acha tu!
 
Back
Top Bottom