Anguko la nchi hizi sasa ni dhahiri

Mshana Jr

Platinum Member
Aug 19, 2012
280,657
729,766
Nazizungumzia Uganda Burundi na Rwand.

Kwanza ni nchi zenye muingiliano wa mengi yanayojulikana na mengi pia yaliyojificha.

Lakini kitakachoziangusha ni u binafsi uroho wa madaraka visasi na hofu ya watawala wa sasa.

Tumeona kilichotokea Uganda kwenye uchaguzi mkuu uliomalizika tumeona ya Burundi, Rwanda bado hali si mbaya sana.

Zimbabwe ya miaka ya 90 ilikuwa inakimbiza kiuchumi, sarafu yao ya Zimdollar ilikuwa na thamani kubwa uroho huu wa madaraka umeifanya Zimbabwe ifike ilipofikia sasa.

Nchi nilizotaja ni wanachama ndani ya jumuiya ya Afrika Mashariki, kuna tatizo kubwa sana tunalifuga hapa mana naona hakuna kuambizana ukweli wala kukemean.

Museveni kashinda kwa hila za wazi kabisa kama ilivyokuwa hapa kwetu, lakini sikuona ndani ya jumuiya akikemewa na yeyote.

Mbaya zaidi tumeikaribisha Sudan kusini kwenye huu umoja, matatizo ya Sudan kusini yanaeleweka yanafanana kwa kiasi kikubwa na nchi nilizotaja
Kuwa na washirika wa namna hii ndani ya jumuiya sidhani kama ni jambo lenye afya sana.

Tuwe makini tusije kupumbazwa na umoja wenye maslahi binafsi toka kwa viongozi wetu.

Ni Kenya pekee ndio wanaweza kusimama kifua mbele na kujivunia demokrasia na usawa ni wao tu ambao chama kilichopo madarakani ni chama cha upinzani, kwengine kote upinzani unaminywa kwa nguvu ya ajabu na ukatili mkubwa mno.

Anguko lolote kwenye hizo nchi litakuwa na athari za moja kwa moja ndani ya jumuiya

TUJITAFAKARI
 
Ndege wafananao huruka pamoja.....
 


Wewe Mshikaji ni pussy! Yaani kwako wewe upinzani kuongoza nchi ndiyo demokrasia?
 
Hapoo ndipo utagundua seraa za Donald trump kuhusu Africa zina umuhimu

tena bila aibu ccm wanmpongeza M7 huu upuuzi kweli
Maslahi ya Museveni Sudan kusini yanaeleweka wazi..anapanua himaya yake kwa namna zote awezavyo, Kagame kwa Burundi. ...ni umoja uliojaa migogoro kati ya nchi jumuiya wanachama , kuna kuoneana na kufanyiana fitina kwingi tuu
Kimsimgi huu ni umoja wa washindwa wenye kuwakilisha maslahi binafsi zaidi hasa ya kisiasa kuliko wananchi
 
Hizo nchi zote zilikuwa na falme mbali mbali chini ya kitu kiitwacho Bahima Empire,Hicho ndicho kinachozisumbua nchi hizo kwa maana ya ukoo fulani ndio unapaswa kutawala.Kenya pia bado wana tatizo hilo,Hapa kwetu J.K.Nyerere aliliona hilo mapema na kulipiga vita mapema sana.
 
 
Inawezekana kabisa kuwa hii ikawa ni coincidence lakini future will tell
 
Kuna haja ya kuchimbua zaidi kuhusu hili
 
Kweli nchi hizi tatu kuingizwa kwenye EAC ilikuwa ni pre-mature. Zingepewa observer status mpaka siweke viziri nyumba zao kwanza. Lakini sikubalinani na wewe kuhusu Zimbabwe. Kilichoiangusha Zimbabwe siyo siasa bali ni kutenda kinyume na matakwa ya mataifa makubwa, hasa walipotwaa mashamba ya wazungu. Vikwazo viliwekwa hili kuiadhibu serikali ya Mugabe na kuzipa somo nchi jirani za South Africa na Namibia ili ziepuke njia ya Zimbabwe. Mugabe alikataa kukiuka ahadi alizowapa wapigania uhuru wenzake za kurudisha ardhi iliyoporwa na wazungu kwa Wazimbabwe wazalendo. He has paid the price. But Zimbabwe will rise again. Pamberi ne Chimurenga.
 
Nina mashaka mno Magu ana vinasaba vya hao wenzake
Ondoa mashaka ndugu...na yeye ndio wale wale...angekuwa nj mpenda demokrasia angemkemea Mu7 anachomfanyia Kizza kule Uganda......
Hawezi kumkemea kwa kuwa anachokifanya Museveni ni sawa na kinachofanywa na serikali yake huko zanzibar au kuhusu uchaguzi wa meya wa jijini dar.....

Wote ndio wale wale....
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…