Tetesi: Amos Makala anahujumu fedha za serikali kulipa fadhila

MFOURSEE

Member
May 15, 2014
12
8
Kwa kweli mkuu wa mkoa wa Mbeya ana matumizi mabaya ya fedha za serikali.

Taarifa zilizotufikia hivi sasa kutoka huko Moshi ni kuwa amewaalika waandishi wa habari ambao aliwateua wawe wakifanya kazi zake kwenda kumtembelea huko Mbeya alikohamishiwa na rais Magufuli.

Taarifa ni kuwa Makala amelipia gharama zote za waandishi hao ambao ni wengi lengo ni kuwapongeza kwa kumuandika vizuri mpaka rais akambakisha kazini.

Taarifa ni kuwa kila mmoja wa waandishi hao maarufu kama timu Makala Kilimanjaro, ambao idadi yao haijajulikana ni kuwa atapata shilingi milioni moja kwa kwenda kutalii tu huko jiji la Mbeya.

Ikumbukwe wakati akiwa Kilimanjaro, Makala alikuwa akilaumiwa kichinichini kwa kuwalazimisha wakurugenzi wa halmashauri za mkoa huo wawalipe waandishi aliokuwa akiandamana nao, leo anawalipa fadhila kwa kuwaalika waende kumtembelea huko Mbeya kwa gharama za serikali, hivi wakuu wote wa mikoa wangefanya hivyo hii nchi itakuwaje?

Hebu fikiria kuwasafirisha waandishi wote hao na taarifa ni kwamba kila mmoja atalipwa shilingi milioni 1 katika safari hiyo mbali na malazi na chakula gharama ambazo pengine halmashauri za huko Mbeya ndiyo zitawalipa.


Mkuu wa mkoa wa Mbeya, Amos Makala.
 
Kama si story tu weka hata viashiria vya ushahidi juu ya haya uyasemayo...Maana kila mkuu siku hizi ana timu yake yawezekana na wewe uko timu mnaolipwa kumchafua makala...
 
Hii unasema wewe kwa niaba yake au, tunadhibitishaje habari hii Kama ni ya kweli na sio kunzushia.
 
Jamani muogopeni mungu hizi zama sio za kutengenezeana scandal kwa nn watanzania tunapenda kuharibiana namna hii weka ushahidi bas mkuu
 
Unawezaje kuthibitisha kama amewaita kweli?Na kama amewaita unatushawishi vp kama atatumia fedha za umma na sio zake?Nakama ni fedha zetu je ameshakamilisha taratibu za kuzitoa benki ama bado na kama tayari ameshirikiana na nani?Toa majibu
 
Jamani muogopeni mungu hizi zama sio za kutengenezeana scandal kwa nn watanzania tunapenda kuharibiana namna hii weka ushahidi bas mkuu
Habari hii inanikumbusha wimbo wa Franco Rwambo Makiady na Sam Mangwana, Mulongo na mulozi ni watu wa kuchoma.
 
hii habari yako inapepea haina mashiko kabisa yani. bila hata ka ushahid ka kufoji
 

Wacha mtimanyongo wewee! Amos Makala ni mmoja wa ma-RC majembe haswaa katika serikali ya JPM. A big up Makalla; wenye wivu wajinyonge!
 
Cookies are required to use this site. You must accept them to continue using the site. Learn more…