thesym
JF-Expert Member
- Aug 15, 2012
- 3,827
- 4,757
Hapo kwenye wapalestina na waisrael kuwa ndugu ebu fafanua kidogo.Kwanza kabisa bwana Eden Kimario asili ya Waebrania wote ni nchi ya Iraki ambayo kipindi hicho iliitwa ufalme wa Uru. Huu ufalme ulikuwa chini ya Wakaldayo na Abrahamu alikuwa Mkaldayo.
Ushahidi wa hili ulithibitishwa na mwanahistoria wa Kiingereza Professor J.E Taylor ambaye aliuchimba huu mji mnamo mwaka 1919.
Tena wewe unavyosema kwamba Wayahudi siyo uzao wa Abrahamu napatwa na ukakasi hasa pale unaposhindwa kufuatilia mambo kwa undani na kuzama juu juu tu.
Neno WAYAHUDI au JEWS linatokana na neno JUDEANS ambao yalikuwa makabila ya YUDA na BENJAMINI yaliyounda ufalme ya YUDA mwaka 931 K.K baada ya Mfalme JEDIDIAH kufariki.
Neno WAYAHUDI lilikuwa linatumiwa sana na WARUMI ambapo walilitumia kuwatenganisha wazao wa Ufalme wa YUDA waliloridishwa kutoka utumwa wa Waajemi. Hili lilitumika ili kuwatenganisha na kabila Wasamaria ambao walichanganyika pamoja na watu wenye asili ya ufalme wa Ashuru (Assyrians). Wayahudi walijitenga pamoja na Wasamaria kwasababu walikuwa wanaabudu dini za kipagani na huku wakimuamini YAHWEH kama ilivyoandikwa kwenye Torati. Na Wayahudi waliamini ni wao pekee ndiyo wana haki ya kutoa sadaka kwa JEHOVAH na siyo watu wengine; hivyo waliwachukia sana Wasamaria.
Ukisoma Torati yote hakuna sehemu ambapo neno WAYAHUDI limetajwa, ila ni Waebrania, Wana wa Israel na WANA WA YUDA na siyo WAYAHUDI.
Kitu cha muhimu kukumbuka ni kwamba Ufalme wa Israel uliundwa na makabila kumi na mawili ambao ulikuwa ni uzao wa Yakobo ambaye YAHWEH alimpa jina ISRAEL. Katika watoto wa Yakobo hakuna kabila la YUSUFU ila watoto wake wawili ambao ni EPHRAIM na MANASSEH.
Sasa ikumbukwe kwamba YUSUFu alipouzwa Misri alipewa mke na Farao. Mke wake alikuwa anaitwa ASENATHI ambaye alikuwa ni mtu wa MISRI. Ufalme wa Misri ulikuwa na wa watu WEUSI hivyo ASENATHI alikuwa ni mtu MWEUSI. Hivyo taifa la ISRAEL lilikuwa na mchanganyiko wa damu nyingi.
Lakini wewe umeona Wayahudi kuchanganyika na Wazungu wa Ulaya Mashariki ni tatizo sana hadi utake kuamini falsafa za kupuuzi zianzoendeshwa hapa duniani. Halafu unaongopa ulivyosema taifa la sasa la Israel linatengenezwa na ASHEKINAZI Jews pekee, hili siyo kweli hata kidogo.
Kuna Wayahudi ASHEKINAZI hawa walitokea Ulaya Mashariki kwenye Ufalme wa KHAZAR; kuna Wayahudi SEPHARDIM hawa walibaki Palestina baada ya Wayahudi kufukuzwa na Masultani wa Kiarabu; kuna Wayahudi FALASHA ambao walikuwa wanaishi kwenye utawala wa SHEBA, ABYSSINIA au ETHIOPIA.
Hawa wote rangi hata maumbile ya mwili zimetofautiana lakini baada ya kupimwa DNA wamekutwa wana undugu mkubwa kuliko unavyotaka wewe kutuaminisha. Mbali kabisa WAYAHUDI wako dunia nzima mfano mkubwa wa makabila ya KIYAHUDI duniani ni:
Na haya yote yamefanyiwa sana uchunguzi na wanasayansi wa mataifa mbalimbali.
- IGBO huko Nigeria.
- WAHINDI WEKUNDU wa Colorado huko Marekani.
- WAHINDI WA KERALA, MUMBAI, KARACHI huko INDIA. (Kati ya hawa kuna wafanyabiashara wengi wa mfalme JEDEDIAH)
- BAADHI YA NEGROES wa Marekani ni WAYAHUDI walioishi katika ufalme wa MALI.
- WAAJEMI WENGI WA IRAN ni WAYAHUDI kutoka PARTHIAN EMPIRE.
Sasa kuchanganyika kwa Wayahudi na Wazungu kuwaje tatizo kwako leo?
Wewe mama yako akiwa ni Mchagga baba yako akawa Mkinga wewe utaitwa MCHAGGA?
Najau WAZAYUNI wanaharibu dunia lakini tusitumie hii fimbo kuwachukia hata WAYAHIDI wasio na hatia bila sababu. Huwezi kumkatalia mtu urithi wake hata kidogo WAYAHUDI na WAPALESTINA ni ndugu kuliko wewe unavyodhani.
Hili huwezi badilisha hata kidogo na Ukweli utabaki kuwa hivyo.