Alex Msama, Mmiliki wa Gazeti la Dira Amwangukia Mwakyembe na kumuomba radhi. Amtimua kazi Mhariri

Walishauza gazeti mtaani kwa vichwa vya habari potofu in the name of politics. Ndiyo maana gazeti la Jamhuri linapongezwa na wasomaji for true investigative journalism. Limeandika matukio mengi na yote yana ushahidi na uchunguzi wa kutosha.:)
Tena hili gazeti la Jamhuri limepongezwa mpaka na watawala na wapinzani. Hawa Dira hakika walikuwa na lengo la kuivuruga nchi
 
Enzi za ujanja ujanja zimepita lakini bado watu wanafikiri ni utani....mtaumia bure
 
Kwakweli nami Nampongeza Msama kwa kuwa muungwana na niwazi atasamehewa na hata gazeti lake linaweza lisifungiwe!

Huu ndio uungwana
Mtu mzima akivuliwa nguo huchutama. Ndivyo alivyofanya Msama. Maana Mwakyembe alichafuliwa sana
 
Alex Msama Amwangukia Mwakyembe Kumuomba Radhi Baada ya Gazeti ya DIRA Analolimiliki Kuchapisha Habari Zenye Utata


1.jpg

MFANYABIASHARA Alex Msama amemuomba radhi Waziri wa Sheria na Katiba, Dk. Harrison Mwakyembe kufuatia habari mbili zilizochapishwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania analolimiliki.

Akizungumza leo na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Msama alisema amejiridhisha kuwa habari hiyo iliyobeba kichwa cha habari ‘Utapeli wa Mwakyembe wamwagwa hadharani’ haikufuata misingi ya uandishi wa habari.

Habari nyingine ambayo imeonekana kumchafua Dk Mwakyembe ni ile ya Mwakyembe atuhumiwa kutapeli bilioni 2 ambazo zimemuumiza kiongozi huyo.

Alisema yeye kama mmiliki wa gazeti hilo amesikitishwa na habari hiyo na kwamba hatua ya kwanza anayoichukua ni kumuomba radhi Waziri Mwakyembe.

Msama alisema sambamba na kuomba radhi atamfikishia barua Mwakyembe ya kumtaka radhi kwa tukio hilo.

“Nimesikitishwa na habari hii kwa kuwa haikuzingatia misingi ya uandishi wa habari, ilihukumu na kuonyesha kuwa lengo lake lilikuwa kumharibia jina Waziri Mwakyembe, ninachukua nafasi hii kumuomba radhi nikiwa mmiliki wa gazeti hilo,” alisema Msama.

Aidha Msama alisema hatua nyingine anayochukua ni kumsimamisha kazi mhariri wa gazeti hilo, Mussa Mkama kwa kuwa alishindwa kufanya kazi yake kwa umakini ya kuhakikisha habari anazozipitisha zinafuata misingi ya uandishi wa habari na weledi.

Alisema Mkama alipaswa kuhakikisha anafuata weledi lakini alishindwa kufanya hivyo kwa hiyo anamsimamisha kazi na kwamba hatua nyingine kali za kinidhamu zitafuata.

“Mimi ni mfanyabiashara sijui mambo ya uandishi, nilimuajiri nikiamini atasimamia yale aliyofundishwa chuoni, kwa kuwa ameshindwa inabidi akae pembeni kwanza,” alisisitiza Msama.
Ameahidi kuwa katika Gazeti la Dira ya Mtanzania litakalotoka Juni 27, kwa ukubwa uleule atamuomba radhi Waziri Mwakyembe.

Hivi karibuni Waziri Mwakyembe aliitisha mkutano wa waandishi wa habari mjini Dodoma akilalamikia kuwa habari mbili za gazeti hilo iliyochapishwa na Gazeti la Dira ya Mtanzania la Juni 20 na la Juni 23 mwaka huu zililenga kumchafua na kuahidi kuwa atalishtaki kupitia habari hizo mbili.

Chanzo: Mpekuzi
Mbona omben Sefue hakumuomba msamaha?
 
Hiyo samahani hajaomba Mwandishi ameomba mmiliki wa gazeti ambaye hana taaluma yoyote ya uandishi.

Hivyo usishangae Mwandishi akifungwa mdomo kwa maslai ya kisiasa hata anaushaidi wa kutosha.
Huyo Mwandishi na Mhariri bado wana kesi yao kule Kisutu. Naamini pia na Mwakyembe hataishia kuombwa radhi bali atachukua hatua za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo
 
Huyo Mwandishi na Mhariri bado wana kesi yao kule Kisutu. Naamini pia na Mwakyembe hataishia kuombwa radhi bali atachukua hatua za kisheria ili kukomesha vitendo hivyo
Nimemuonea sana huruma Msama maana hawa wandishi na wahariri wake watamponza maana naiona hatari ya gazeti lake kufungiwa! Bila shaka Mwakyembe atamsamehe!
 
Shida ya wafanyabiashara waoga ndo hiyo nafikiri biashara ya habari haiwezi akauze vitumbua.

Ningemwelewa kama mhariri ndo angesema hayo na si vinginevyo. Wapi jukwaa LA wahariri tusikie kauli yao juu hili LA mmiliki kutokea hadharani na kuiponda story za mhariri wake

Kwa watu makini hatua hii inaathari nyingi moja ikiwa ni kuua sifa ya gazeti husika.

Lakini pia mwakyembe no mwanahabari aliyesomea na kufanya hiyo kazi, je aliwasiliana nna mhariri kabla ya kutoa vitisho hivi?
 
Naona issue imemalizwa juu kwa juu na watanzania wasiofikiri kwa kina mambo kama kina Lizabon wameridhika .
 
Lazima alipe fidia toba haitoshi, kwasabu uzushi huu ulifanya magazeti yake kununuliwa sana jambo lilimpa faida na sasa asije kwa gia ya radh wakati alipo mchafuwa alijuwa anapata nini. Dr usikubal maneno bila fidia iwe adhabu kwa wajinga wote walio mtuma.
 
Back
Top Bottom