Ajali yaua 29: Mabasi ya Kampuni moja ya City boy yagongana Singida, ni basi la Dar na Shinyanga

City Boy Express zilizogongana zote ni za route ya Dar- Kahama. Moja ilikuwa intoka Kahama nyingine inatoka Dar. Hawana route ya Mwanza.


Pole kwa wahanga wa ajali hii. Kwa taarifa nilizopata ni kuwa ajali imesababishwa na style ya kusalimiana ya madereva hao. Wanabadilishana lanes...sasa leo mchezo wao umegeuka balaah kubwa.
Kuna City boy zinaenda Mwanza
 
Hii inatisha sana!! Sasa hao madereva akili zao zilikuwa sawa? Pia na hii kukamatwa na mitochi kila km 10 nadhan inachangia kwani madereva wanakuwa na stress sana wakati wakiendesha!! Haisaidii ila inaongeza tatizo!! Mtu amepigwa penalty zaidi ya nne unafikiri kichwa kinakaa sawa??
 
Kwa kweli ni shida,nilisafiri na basi moja kueleke mikoa ya kusini.yaani wana basi 4 kwenda 4 kurudi.njiani anaekuwa kwanza akipita eneo lenye tochi anawataarifu wenzake kuwa ukifika eneo fulani kuna tochi ubane,ukishapita mwagika mpaka eneo fulani kuna tochi nyingine.nauliza kama serikali ipo serious na maisha ya watu ule utaratibu wa police mwenye sare kusindikiza mabasi upo wapi?inasikitisha sana serikali inaacha mambo ya msingi inahangaika na SHISHA.
 
Poleni sana wafiwa wote ajali mbaya ambazo nyingi zinasababishwa uzembe wa madereva
 
City Boy Express zilizogongana zote ni za route ya Dar- Kahama. Moja ilikuwa intoka Kahama nyingine inatoka Dar. Hawana route ya Mwanza.


Pole kwa wahanga wa ajali hii. Kwa taarifa nilizopata ni kuwa ajali imesababishwa na style ya kusalimiana ya madereva hao. Wanabadilishana lanes...sasa leo mchezo wao umegeuka balaah kubwa.
Inasikitisha sana kama walikuwa wakifanya hayo manjonjo huko nyuma na abiria hawakuwahi kuwakemea au kuwareport popote. Abiria wawe na utamaduni wa kukemea na kuwareport madereva wanaoonesha tabia zisizofaa wawapo safarini. Inauma sana kupoteza maisha ya watu. RIP Marehemu.
 
Nimeishudia nihatari sana
Ajari imesababishwa na madeleva kwasababu walikua speed halafu wakatoa mikono kusalimiana dilishani gari moja likamisi na kumvaa mwenzie kilicho tokea nimeona watu wengi wakiekwa kwenye scania lamzigo wakiwa wamekufa mungu atrehemu
 
Michezo ya kupenda kuovateki kila mara barabarani haya ndio matokeo yake.
R.I.P marehemu
 
Hao madereva wa City Boy huwa wanamchezo wakikutana wanasalimiana kwa kubadilishana upande wa kupita yaani wakulia atapita kwa mwenzie kushoto na wakushoto atapita kwa mwenzie kulia tena kwa speed ileile.
Sasa nafikili kilicho fanyika leo ni kukosea mahesabu na mmoja kuchelewa kuhama upande wake kwenda kwa mwenzie ndio wakaingia uso kwa uso.
Picha ni za kutisha na kusikitisha sana
 
Back
Top Bottom