mimiamadiwenani
JF-Expert Member
- Mar 9, 2022
- 5,637
- 7,575
Jambo Tanzania!
Hawa wadogo zetu waliomaliza hasa kuanzia mwaka 2015 kuja juu, wana hali mbaya sana. Siyo ya kiuchumi, hata ya kihisia.
Naona hali halisi na nina baadhi nawafahamu kwa mbali, wanapitia kipindi kigumu sana cha msongo wa mawazo.
Mitaani wanakoishi wamegeuka kuwa 'topic' na watu wa kutolewa mifano. Wazazi wanawaonya watoto wao na kuwaingiza graduates kwenye mazungumzo yao.
Watoto wanakataa shule kwa kuwanyooshea vidole gradautes, kuwa kusoma ni kupoteza muda.
So sad!
Kubwa zaidi ni hili, kipindi hiki kila mtu hata yule ambaye hajasoma na anabangaiza maisha kama wewe, naye anajifanya kukupa ushauri na kukukalisha chini.
Mbaya zaidi anasahau ya kwake yeye, anaingilia na yako. Kipindi hiki hata mtoto mdogo tu kuliko wewe anakukalisha na kukupa ushauri wa maisha, mtoto ambaye alitakiwa achukue ushauri kutoka kwako.
So sad!
Hakuna kipindi unachotakiwa kuwa na roho ngumu kama hiki. Kaka zenu tuliwahi kupitia huko back in years ila mambo yakakaa sawa.
Ukweli ni kwamba, hakuna aliye kwa ajili yako graduate. Kuanzia primary school, secondary, high school, mpaka chuo, kote huko wakufunzi walikudanganya sana.
Kila mmoja yupo kwa ajili ya familia yake na walio wa kwao, wakufunzi wakakuficha hili. Wao wakakuambia tu soma uwe mara daktari, mara rubani, mara mhasibu, na kadhalika.
Sasa hujachelewa, futa mentality hiyo ya hapo juu. Jitenge na watu unaofanana nao, jitenge na walala hoi wasio na future mbeleni, na ujitenge na wale ambao wanabangaiza kama wewe ila wanajifanya kukushauri kuhusu maisha huku wakikucheka kisiri siri.
Kaa na watu potential, jipendekeze kwa tija, kaa kwa tija. Kama ni kuzurura basi zurura mitaa potential ambayo utakutana na watu potential. Unazurura Kimara, sijui Tandale mara Buza ili upate nini?
Nenda bandarini, nenda Mikocheni, nenda Masaki, Msasani, nenda Posta nk.
Ukitaka kunukia, kaa karibu na uwaridi.
Yangu ni hayo wadogo zangu. La mwisho, usidhani kuna watu wanasikitika kuhusu hali yako, hakuna. Kama wapo basi ni wazazi wako na ndugu wachache wa damu, BASI.
Watu wanafurahi na wanapenda kukuona ukiwa hivyo hivyo jobless, mchafu mchafu, huna ramani, hueleweki, hujiamini, na hupigi hatua yoyote. Huo ndiyo ukweli wa maisha.
Atakayekuwa bega kwa bega nawe kwa wakati huu, ukipata kivuli usije kufanya blunders na kumsahau.
Aluta continua!
Endeleeni kunywa mtori nyama zipo chini.