Mimi niliwaandikia mpaka email, wakijifanya kunipigia na kubisha. Niliambatanisha mpaka na screenshot ya sekunde kumi wanazokula badala ya moja iliyotumika lakini bado wakabisha na kujifanya kutumia lugha za uongo. Walipoona napuuzia simu zao wakatuma msg kuwa tatizo lako limerekebishwa wakati kiukweli hakuna kurekebishwa kokote. Wengi wanapuuzia kuona ni sekunde chache lakini kama kwa siku wakiwaibia wateja mil. 3 sekunde 9 unadhani wanajipatia kiasi gani kwa udanganyifu.
TCRA badala ya kufuatilia watu wanaomuita baba j majina ya kumtusi ni bora wangetetea haki zetu watumiaji wa simu. Airtel ni jipu kubwa mno linalopaswa kutumbuliwa.