KARLO MWILAPWA
JF-Expert Member
- Apr 10, 2019
- 2,717
- 4,896
Kwa mara nyingine tena nasikitika kuona kuna upotoshaji kwa ahadi ya milioni 50 kwa kila kijiji iliyopo kwenye ilani ya uchaguzi ya CCM ya mwaka 2015. Kuna wengine kwa makusudi kabisa wameamua kuipotosha ahadi hiyo ili ionekane kwamba zile milioni 50 ni kwa ajili ya kugawiwa bure na si kuleta maendeleo.
Siku chache zilizopita Katibu mkuu wa CCM ambaye ndiye msimamizi mkuu wa utekelezaji wa ilani ya uchaguzi ya CCM ya 2015 ambayo ilitoa ahadi ya milioni 50 alisema ahadi ya milioni 50 imeshatelekezwa kupitia utekelezaji wa miradi ya maendeleo na sera ya elimu bure. Kwa kauli hii ya Katibu Mkuu ni kwamba serikali ya CCM imeangalia picha kubwa kwa utekelezaji wa ahadi ya milioni 50 kwa maslahi ya wengi.
Kwa ujenzi wa vituo vya afya, ujenzi wa shule, utekelezaji wa sera ya elimu bure na miradi mingine ni wazi kwamba ahadi ya milioni 50 kwa kila kijiji imetekelezwa kwa manufaa ya wengi na maslahi mapana ya taifa. Wengi wanachoshindwa kujua ni kwamba ilani haina mipango na mipango ya utekelezaji wa ilani inawekwa na serikali. Ahadi ya million 50 ya kwenye ilani mpango wake wa utekelezaji ndio kama huo aliosema Ndg. Katibu mkuu wa CCM.
Upotoshaji wa kuaminisha wananchi kuwa ahadi ya milioni 50 ilikuwa ni kwa ajili ya kupatiwa hizo pesa au kugawiwa tu kwa wanakijiji bila kuelekezwa kwenye shughuli za maendeleo ni wa kupinga. Kuna mtu anadiriki kuaminisha watu kwamba ahadi ya milioni 50 ilikuwa ni kugawiwa kwa wananchi, namnukuu ‘…kama hukupata mshiko wako labda wanakijiji wenzako wamekudhulumu’. Huu ni upotoshaji mkubwa na CCM haikuwahi kutoa ahadi ya kugawa pesa kwa wanakujiji ila kutumia hiyo million 50 kuboresha maendeleo ya wanakijiji