Erythrocyte
JF-Expert Member
- Nov 6, 2012
- 125,690
- 239,249
Lakini kwanini mambo haya yamekuja ghafla hivi?
Taarifa kamili hii hapa.
=====
Hospitali ya Aga Khan kwa kushirikiana na Shirika la Reconstructing Women International (RWI) na Hospitali ya Taifa Muhimbili, inatarajia kufanya upasuaji kurekebisha maumbile kwa wanawake na wasichana 25 kutoka maeneo mbalimbali nchini.
Upasuaji huo utakuwa bure na unatarajia kuanza kesho Jumanne Novemba 28 hadi Desemba 2, 2023 ukiwa na lengo la kurejesha uwezo wa kutembea kwa watu ambao wanamatatizo yaliyotokana na majeraha makubwa ya moto, ajali za barabarani kasoro za kimwili na wahanga wa ukatili wa kijinsia.
Upasuaji utasimamiwa na timu ya madaktari wa kimataifa wa upasuaji wa kurekebisha maumbile kutoka Marekani, Canada, na Ulaya wakishirikiana na madaktari wa Hospitali za Aga Khan Dar es Salaam, Muhimbili, Bugando, na Mnazi Mmoja ya Zanzibar.
Daktari Mwandamizi wa Upasuaji wa Aga Khan, Dk Athar Ali amesema programu hiyo ambayo kwa mwaka huu ni ya nane tangu kuanza kwake inalenga kurejesha utendaji wa kimwili ili kuwezesha na kuboresha maisha ya wanawake na wasichana wa Tanzania.