A
Anonymous
Guest
Habari ndugu zangu Wana JamiiForums, ninaomba kusaidiwa suala hili
1) Hivi Sheria za nchi zinaruhusu mfungwa kuendelea na wadhifa wake kazini au ni huku Kwetu Iramba tu?
Ninaleta mada hii kutoka kata ya Kyengege wilaya ya Iramba mkoa wa Singida. Katika kata yetu Afisa Mtendaji wa Kata alikamatwa kwa rushwa na kesi iliunguruma mahakama ya wilaya Kiomboi na hukumu weo huyu maarufu kwa jina la Makala alipatikana na hatia na kuhukumiwa kifungo cha nje mwaka mmoja na kulipa faini sh 200,000 ambazo alilipa. Nijuavyo mimi mtumishi wa umma akipatikana na hatia anakuwa amepoteza sifa ya kuwa mtumishi, hivi Sasa anatumikia kifungo cha nje wakati anaendelea na kazi.
Tunaomba mamlaka husika zifuatilie suala hili maana limetuacha midomo wazi kata ya Kyengege, kata ya bwana Nchemba na ni kata ya mwenyekiti wa halmashauri bwana Inosent, hatuna uhakika kama wanamlinda au na wao hawalijui hili
Natumaini mamlaka mtashughulikia haraka iwezekamavyo
Asante