Zitto
Former MP Kigoma Urban
- Mar 2, 2007
- 1,562
- 10,886
Hotuba.
Ndugu Watanzania,
Nichukue nafasi hii kumshukuru Mwenyezi Mungu kwa kutujalia uzima na afya uliotupa nafasi ya kuzungumza leo.
Mwaka uliomalizika ulikuwa na changamoto nyingi sana kwa ujumla ulikuwa mwaka mbaya kwa maeneo muhimu ya demokrasia, Utawala Bora, Uchumi na Maendeleo kwa ujumla.
Tumeshuhudia kukithiri kwa matukio ya utekwaji na ubambikiwaji wa kesi kwa wakosoaji wa serikali, kudhulumiwa kwa wakulima wa korosho, kuporomoka kwa uchumi na hali ya Watanzania kukosa Furaha.
Tanzania sasa inatajwa kama mojawapo ya nchi ambazo wananchi wake hawana furaha kabisa na sababu zinajulikana.
Eneo pekee ambalo kidogo lilitupa furaha kidogo ni ushiriki wetu kwenye Mashindano ya AFCON nchini Misri na mafanikio ambayo wanamuziki wa nyumbani kama Diamond, Ali Kiba, Nandy na wengine wamekuwa wakiyapata katika eneo la sanaa.
Nawapongeza kwa mafanikio waliyopata ingawa najua pia BASATA imeendelea kuwa kikwazo kwao na bado kuna matishio dhidi yao na ushahidi ni kuhusu mwanamuziki Roma ambaye sasa anaishi Uhamishoni akihofia hatma yake.
Watanzania Wen zangu, nijikite sasa kwenye changamoto zetu.
1. Uchumi
Kulinganisha na mwaka 2015, hali yetu ni mbaya. Achaneni na propaganda za Ndege na porojo nyingine.
Uchumi wetu unaporomoka. Mwaka 2015 kila Mtanzania alikuwa anadaiwa shilingi 920,000 leo hii kila Mtanzania anadaiwa shilingi milioni 1.2.
Deni la Taifa linaongezeka kwa kiwango cha Sh trilioni nne kwa mwaka ambacho hakijawahi kutokea kwenye historia ya Taifa.
Si mara ya kwanza kwa Tanzania kununua Ndege, kujenga madaraja, hospitali au mabwawa ya Umeme... Tumekuwa tukifanya hivyo kwa miaka yote tangu kupata Uhuru.
Lakini hatukuwahi kukopa namna hii tena kwa riba kubwa katika Benki za kibiashara za kimataifa au benki za ndani. Uchumi unavurugika kwa sababu fedha yote inapelekwa nje ya nchi.
Ajira nazo hakuna. Mamilioni ya vijana wanaingia kwenye soko la ajira kila mwaka lakini ajira zilizopo ni 70,000 tu.
Hili ni bomu linalohitaji maarifa makubwa kulitegua na kwa bahati mbaya si Rais Magufuli wala CCM mwenye uwezo wala maarifa ya kutegua.
Kilimo kimevurugwa. Wafanyakazi hawaongezwi mishahara, wastaafu hawapati mafao na idadi ya wagonjwa inaongezeka.
Mwaka jana pekee, watu nane katika kila watu 10 walikwenda kwenye vituo vya afya kutibiwa. Hii inakupa picha ya hali ya afya zetu ni mbaya kiasi gani.
Mbaya zaidi, serikali imekuja na Mpango wa Bima ya Afya ambao lengo lake ni kugeuza matatizo ya kiafya ya Watanzania kuwa mtaji wa kuchuma pesa wa serikali.
2. Tunataka kufanya nini
Mwaka 2020 ni mwaka wa uchaguzi. Watanzania watapata tena nafasi ya kuchagua viongozi wa kuwatawala kwa miaka mingine mitano.
Tunajua serikali hii haitaki upinzani. Tumeona usanii ilioufanya kwenye Uchaguzi wa Serikali za Mitaa. Tunaamini watataka kufanya tena uhuni mwaka 2020.
Ni jukumu la Watanzania wote kuhakikisha kwamba mwaka 2020 watu wanashiriki kuchagua wagombea na vyama wanavyovitaka.
ACT Wazalendo tumejiandaa kukabiliana na changamoto zinazowakabili Watanzania sasa na baadaye.
Tuna mikakati imara ya kuuzimua na kukuza uchumi wetu ili uwe suluhisho la changamoto zetu.
Tunajua kwamba mwaka 2025 kutakuwa na watoto wengi zaidi wanaoanza shule, vijana wengi zaidi wanaotafuta ajira na uchumi unatakiwa kujibu changamoto hizo.
CCM imeshajichokea. Rais Magufuli amethibitisha kwamba hana maarifa wala Uwezo wa kututoa hapa tulipo.
Tuungane kwenye kuiondoa CCM hii madarakani. Ndiyo namna pekee ya kusalimisha mustakabali wa nchi yetu na watoto wetu.
Kama unataka kuishi katika nchi ambayo watoto watapata Elimu bora, vijana watakuwa na uhakika wa ajira, wazazi hawatapoteza watoto wao kwa kutekwa au kubambikiwa kesi, wakulima wanaofaidi jasho lao, wastaafu wanaopata kilicho chao na wafanyakazi wanaoheshimiwa, chaguo ni moja tu; mabadiliko.
ACT Wazalendo iko tayari kuwaongoza Watanzania katika zama mpya.
Nawatakia kheri ya Mwaka Mpya 2020