Sophist
Platinum Member
- Mar 26, 2009
- 4,486
- 3,407
Ndugu, nawashauri tuwe wazalendo. Na uzalendo huu tuuoneshe kwa vitemdo. Hawa jamaa (Wacanada) wa Barrick a.k.a Africa Barrick Gold (ABG) na sasa ACACIA, tangu waanze kuchimba na kuvuna dhahabu mwaka 1999 hadi mwaka jana (2016) hawajawahi kulipa kodi ya makampuni (CIT) asilimia 30 ya faida, kwa madai kuwa walikuwa wakipata hasara. Mwaka jana (2016) serikali iliwaamrisha kulipa kodi hiyo kuanzia mwaka huu wa fadha na arrears za miaka ya nyuma kwa sababu serikali iligundua kuwa licha ya kudai kupata hasara, walikuwa kwa miaka kadhaa ya nyuma, wakiwalipa gawio la faida wanahisa wao. Kampuni hii haiko mahali pengine popote duniani kwa jina hili (ABG/ACACIA) isipokuwa Tanzania. Kwa hiyo faida waliogawia wanahisa wao ilitokana na uzalishaji wa hapa nchini kwetu. Sasa wanaposema kwenye makapi (mchanga) tu wamepoteza mabilioni ya Tzs.kwa wiki 2 na kwenye core resources (dhahabu) wamekuwa wakipata kiasi gani? Heko JPM ukweli sasa utajulikana.