Nionavyo kumbe kuna uwezekano wa watu wawili wanaopata kiasi sawa cha mshahara wakawa wanakatwa kiasi tofauti cha PAYE. Nasema hivyo kwa sababu kwa mujibu wa taratibu kabla ya kupiga hesabu ya PAYE inabidi kwanza utoe michango ya mifuko ya jamii ambapo katika mifuko mingine mfanyakazi anachangia 10% na mingine 5%. Kwa hiyo kama mimi napata gross salary ya Tshs. 1,000,000/= na kama nachangia 10% kwenye mfuko wa jamii PAYE yangu itatoka kwenye 900,000/= wakati mwenzangu apatae gross salary sawa na ya yangu na kama anachangia 5% yeye PAYE itatoka kwenye 950,000/=. Sijui kama niko sawa hapo?