Utafiti: Ndoa nyingi zimeshakufa ingawa watu bado wanaishi kama mke na Mume

Dr Matola PhD

JF-Expert Member
Oct 18, 2010
57,052
94,756
Nitandika Kwa kifupi najuwa mmu watu hawapendi magazeti.

Wazungu unafki huu hawaiwezi, kuishi na mtu eti kisa mna watoto lakini upendo umekufa.

Mi ni mtu wa society Kwa utafiti wangu wa miaka isiyopunguwa 10 nimegunduwa ndoa si kitu muhimu tena Kwa jamii ya Kitanzania, anayebisha hili shauri yake.

Ndoa za Watanzania wengi ni Sawa na Jehenamu kunyimana unyumba na tafrani zote.

Siku nilikuwa mediator ingawa sipendi kabisa kusuruhisha matatizo ya ndoa, findings zangu na ushauri wangu ni huu.

1. Kuoa au kuolewa siyo Jambo la lazima zingatia hili, Mimi nina ndoa lakini sikushauri kuingia kwenye ndoa kama hujui ndoa ni nini.

2. Kuna swala la ulevi Kwa ujumla, hili nimeona linaleta shida Sana kwenye ndoa, wote mmekutana kwenye pombe baadaye unamkataza mwenza wako asinywe pombe, jitafakari Sana hapo.

3. Hili ni tatizo, linawahusu wanawake wote, kumekuwa na tabia ya wanawake kutaka kuwarusha stage za ujuwaji waume zao, kumbe binadamu NI lazima apite hizo stage ili ajuwe mema na mabaya.

Kijana wa miaka 28 mpaka 40 unataka Aishi kama mtu wa miaka 50 kisa amekuwa wewe dada Hilo haiwezekani na likiwezekana elewa umetolewa na zezeta

Solution: Kwenye kupata wenzake , kila mtu ajitahidi kupata choice na quality zake, ukitaka mcha Mungu tegesha makanisani huko nako si kwamba Wana ucha Mungu wowote.

Point hapa vile umemkuta mwenzao wako bila kuangalia tako au uhandsome wake au pesa zake, elewa hivyo ndivyo alivyo usitalajie kwamba wewe utambadirisha, shida kubwa ya ndoa nyingi kuwa ICU ukichunguza Kwa makini utagunduwa tu kuna mwanandia mmoja anaamini yeye ndio mwenye akili mwenzake Hana akili.

Tutaendelea kwenye comment session.
FB_IMG_1712222178739.jpg
 
Ni kheri kuachana kuliko kuishi kwenye mahusiano mfu.
Okoa amani yako ya moyo maisha hayajirudii hapa duniani.
Kukomaa kwenye ndoa mfu ni kujikosea heshima moyo na mtima wako mwenye coz unaweza ukaishi bila furaha hapa duniani na ukifa ukaishia kuchomwa huko Jehanamu au moto wa milele.
 
Huyo ni chaguo lako x 3

Sijui hii nyimbo aliimbaga nani

By the way, Kwa namna hali ya mambo ilivyo Kwa ground hasa Kutokana na push ya haki sawa (50/50) Kuna haja kukawa na Ndoa za mikataba aisee
Siyo ndoa za mikataba tu, Bali Kile kiapo kiandikwe upya.

Kiapo cha ndoa kinasema utamvumilia katika shida na Raha na maradhi, lakini jinsia ya Ke wengi wao kiapo hiki wamekariri kipengele cha wakati wa raha tu.

Kuna Jamaa yangu mmoja ilibidi Mimi niingilie Kati nimwambie mke wake ukweli Jamaa Hana pesa, kuna pesa anaidai kwangu ziko kwenye process ya kulipwa.

Imagine kuna mwanamke hataki kusikia lugha ya kumwambia wiki hii mipango yangu kipesa haiko Sawa kama Una akiba okowa jahazi nyumbani, sasa kuna haja gani ya kuwa na ndoa hapo? Ndoa ya upande mmoja?
 
Ndoa nyingi zinaanza kwa kuunganishwa na mapenzi kati ya mke na mume, lakini baadae mapenzi kati ya wawili hao hufa na ndoa kubaki inaunganishwa na uwepo wa watoto kati ya mume na mke.

Wazungu sijui huwa wanawaandaa vipi watoto wao kisaikolojia kuishi pale ambapo baba na mama zao huachana, huku kwetu watoto mara nyingi hupitia kipindi kigumu sana kisaikolojia pale ambapo wazazi wao hutengana.

Naamini kwa kutambua hili, ndio maana wazazi huamua kuishi pamoja kwa shingo upande ilimradi watoto wabaki na amani yao, na kufanya hivi kwangu sio unafiki, ni uamuzi wa kijasiri kati ya wana ndoa.
 
Umesema sahihi Mkuu

Vyema ushauri wako uzingatiwe
 
Nilishangaa Sana Bill Gates na Melinda Gates kutengana lakini in deep katika utafiti wangu nimegunduwa wazungu hawako tayari kufake maisha.

Ona hawa nao, kituko kingine hiki.
Mkuu,

Picha ya tatu hii umepost na zote Kuna kipengere unakiruka.

Ukisha "attach photo" Kuna neno kule juu kushoto limeandikwa " insert". Ukigusa hapo inakuonyesha maneno mawili, 1. Thumbnail 2. Full image. Gusa full image kisha umemaliza kazi. Picha zitaonekana full kama Uzi wa "warembo worldwide".

Tuendelee na mjadala.
 
Ndoa nyingi zinaanza kwa kuunganishwa na mapenzi kati ya mke na mume, lakini baadae mapenzi kati ya wawili hao hufa na ndoa kubaki inaunganishwa na uwepo wa watoto kati ya mume na mke.

Wazungu sijui huwa wanawaandaa vipi watoto wao kisaikolojia kuishi pale ambapo baba na mama zao huachana, huku kwetu watoto mara nyingi hupitia kipindi kigumu sana kisaikolojia pale ambapo wazazi wao hutengana.

Naamini kwa kutambua hili, ndio maana wazazi huamua kuishi pamoja kwa shingo upande ilimradi watoto wabaki na amani yao, na kufanya hivi kwangu sio unafiki, ni uamuzi wa kijasiri kati ya wana ndoa.
Sisi bado tupo kizazi cha nyani, tutakapotimia kuwa binadamu kamili tutaheshimu thamani ya furaha na thamani ya uhai.
 
Kiapo cha ndoa kinasema utamvumilia katika shida na Raha na maradhi, lakini jinsia ya Ke wengi wao kiapo hiki wamekariri kipengele cha wakati wa raha tu
mtu mzima umekutana naye ukubwani hawezi jali kuhusu wewe, ataonesha upendo long as kibunda kinasoma
ndiyo maana tunasema, Ndoa ni Ajira kwa mwanamke, huna pesa , hutapewa uchi, huna pesa hakuna upendo

achilia mbali ubinafsi walio nao

wajanja wamesanuka, HUO NI UTAPELI
 
Siyo ndoa za mikataba tu, Bali Kile kiapo kiandikwe upya.

Kiapo cha ndoa kinasema utamvumilia katika shida na Raha na maradhi, lakini jinsia ya Ke wengi wao kiapo hiki wamekariri kipengele cha wakati wa raha tu.

Kuna Jamaa yangu mmoja ilibidi Mimi niingilie Kati nimwambie mke wake ukweli Jamaa Hana pesa, kuna pesa anaidai kwangu ziko kwenye process ya kulipwa.

Imagine kuna mwanamke hataki kusikia lugha ya kumwambia wiki hii mipango yangu kipesa haiko Sawa kama Una akiba okowa jahazi nyumbani, sasa kuna haja gani ya kuwa na ndoa hapo? Ndoa ya upande mmoja?
Hii mindset ya wanawake nayo kwa kiasi kikubwa inachangia tatizo, wengi wao hupigania kuolewa wakiamini kwenda kwa mume ni sawa na kwenda kwa "baba zao wadogo", wanakwenda kutafuta malezi mengine nje ya nyumbani kwao walipozaliwa.

Hapa ndio chanzo cha wale jamaa wa kataa ndoa wanapopata nafasi ya kujidai, wanawake wanakuwa wagumu sana (baadhi) kutoa sehemu ya kipato chao kurekebisha mambo nyumbani pale hali inapoyumba, na hata wakitoa, basi ujue utasemwa mpaka ujute.

Mwanaume akiamua kuishi na mwanamke kwenye hizi ndoa zetu, simply hatakiwi kuwa na kisirani, hatakiwi kujiuliza maswali, akae akijua anatakiwa kutoa pesa non stop kila zitakapohitajika, na kama ikitokea akakosa bahati mbaya, ajiandae kwa lawama, sasa ni wangapi wenye uwezo wa kuvumilia hizo lawama?!
 
Back
Top Bottom