fundi radio
Member
- Apr 2, 2023
- 52
- 95
Utangulizi.
Baada ya kuja kwa ubepari , uhuru wa watu kufanya Biashara popote ilichangia kuwa na muingiliano wa wafanyabiashara kutoka sehemu mbalimbali Dunia .
Hapo ndipo walanguzi wakubwa walipopata nafasi kupitisha Madawa ya kulevya, kwenye viwanja vya ndege, mipakani Kwa njia ya Barabara, na Kwa kupitia bandari bubu na bandari za kawaida.
Biashara ya Madawa ya kulevya imekuwa ikipigwa vita Kwa kuwa na athari kubwa kwenye jamii yetu mpaka kuundiwa idara(DCEA) itakayo pambana na kuzuia biashara na matumizi ya Madawa hayo.
Naam ni biashara ya Madawa ya kulevya aina ya cocaine, heroin, inayo fanyika kwenye masoko ya vyakula Katika miji yetu nchini.
Mpango kazi ulivyo.
Kwenye Kila karibu na soko kunakuwa na (pusha), WAKALA wa kuuza Madawa hayo Kwa kupitia vijana umri rika la (27-40), Hawa vijana kazi Yao ni kwenda Kwa pusha kuchukua mzigo na kwenda kuuza mzigo kidogo kidogo.
Kuna vijana wanaoununua Madawa Kwa pusha na kwenda kuyauza Moja Kwa Moja sokoni, na Kuna wengine wanachukua Madawa kama (Malikauli), Yan wanachukua mzigo bila kutoa pesa, alafu wanaenda kuyauza sokoni ,wakisha maliza kuyauza wanapeleka mauzo yote Kwa pusha, alafu pusha anawapa asilimia kadhaa ya mauzo iliyo patikana.
Na vijana wengi wanafanya kazi ya Malikauli, kwani wengi wao hawana uwezo wa kuyanunua Kwa mkupuo.
Na mzigo wanao pewa na pusha hauzidi laki 3, pia inategemea na mahitaji ya soko husika, na uhaminifu wa kijana Kwa pusha.
Hawa vijana wanaweza kuwa wawili au Moja kwenye soko Moja, Hawa vijana wakisha nunua mzigo Kwa pusha huifadhi huo mzigo kwenye nyumba zao wanako ishi ,na kuendelea kuuza mzigo kidogo kidogo.
Je, hawa vijana wakoje?
Ni vijana wanao okotaokota vitu vinavyo anguka masokoni wakati wa kupakuwa mizigo mfano vitunguu , viazi, nyanya,ndizi. Utawakuta wakitembeza vitu hivyo kwenye mifuko midogo, ungo na kuviuza, .
Ila sio wale wabeba mizigo , kwani wengi wa wauzaji ni wabwia UNGA, hawezekani ubwie UNGA alafu ukabebe gunia la viazi la kilo 100.
Je, wanawauzia akina nani?
Wanawauzia watu wa maeneo ya karibu na soko, hasahasa vijana ndio wateja wao wakubwa.
Je, Hawa mapusha wakoje na ni akina nani ?
Ni watu wenye Hali nzuri kimaisha, wafanyabiashara na wengine ni wanaheshimika kwenye jamii, mbaya zaidi Kuna mpaka wa waheshimiwa madiwani. Mapusha ni watu wanao safirisha mizigo Mara Kwa Mara ya aina mbalimbali.
Wana uzoefu wa kusafirisha mizigo, na wanajua njia au Vituo vyote ambavyo polisi wanakuwepo.
Wanatumia usafirishaji wa mabasi ya abiria , ambapo Kwa Sasa wanaotumia sana njia hii ya usafiri , Je ni kwanini Wanatumia usafiri wa mabasi ya abiria
i) mizigo inayosafirishwa kwenye mabasi haikaguliwi Kwa ndani, wamiliki wa mabasi wao wanataka mzigo uwe umefungwa vizuri basi, watakauliza ndani Kuna Nini ,lakini hawataufungua.
ii) Siyo rahisi kuugundua mzigo kwani unakuwa umejichanganya na mizigo mengine.
ii) Namba za simu wanazoweka kwenye mizigo mara nyingi huwa ni za Uongo .
Kibaya zaidi Serikali imeanzisha usafiri wa abiria wa usiku, (wamempiga chura teke).
Je, vyombo vya usalama kinachoindelea kwenye haya masoko?
Masoko karibia yote yamezungukwa na Vituo vidogo vidogo vya polisi, je polisi hawajui kabisa kinachoendelea kwenye haya masoko? Mpaka sisi raia wa kawaida tumesanuka.
Wanaposema biashara ya Madawa inahusisha Baadhi ya viongozi waandamizi wa usalama muwe mnaelewa , haiwezekani MTU anafanya Biashara ya Madawa ya kulevya miaka nenda Rudi na hakamatwi na anajulikana kabisa anaishi sehemu Fulani.
Yani Iko hivi ukisha ingia kufanya kazi ya kusafirisha Madawa ya kulevya na kuuza huruhusiwi kuiacha , Kwa sababu utakapo iacha kufanya kazi hiyo , wenzanko wanajua utaenda kutoa Siri ya biashara Yao.
Je, ni kweli Baadhi ya viongozi wakubwa wanausika ?.
Jibu ni NDIO. Kwa akili ya kawaida TU haiwezekani shehena za madawa ziingie nchini bila kujulikana na wakuu wa usalama, na ikitokea shehena zimekamatwa, ujue mchongo umesanuka na watu wengi mpaka Interpol wanajua, Kwa hiyo kuua kesi , wanaamua kutengeneza skendo, kwamba taasisi imekamata shehena za madawa, kumbe mweee , bahati TU mbaya mchongo ulivuja.
Biashara ya Madawa ya kulevya inavyofanywa kwenye minada.
Ni Ile minada ya vitu vya majumbani, nguo, ambapo wafanyabiashara kutoka wilaya tofauti au mkoa husafiri Kwa ajili ya kwenda kufanya Biashara.
Minada hii huwa Kuna mkusanyiko wa watu wengi kutoka sehemu tofauti, wanakutana kuja kufanya Biashara sehemu Moja.
Sasa kutokana na kusanyiko la watu wengi , Kila mtu akiwa na harakati zake za kijipatia kipato .
Wafanyabiashara wa Madawa ya kulevya wameitumia hii fursa ya wao ya kusafirisha Madawa na kuyauza maeneo hayo.
Na hiyo biashara Inakuwa ni ya Malikauli, pusha anampa kijana wake mzigo akauze kidogo kidogo alafu baadae ampekekee fedha.
Athari ya hii biashara kwenye jamii yetu.
I) Mmomonyoko wa madili kwenye jamii yetu, mfano vitendo vya ubakaji, wizi, ukawiti , Kwa kiasi kikubwa kinafanywa na wanaotumika Madawa ya kulevya.
ii) Maambukizi ya magonjwa kama ukimwi, sindano za kijidunga wanazoshirikiana pamoja, Sina sababisha maambukizi ya ukimwi.
iii) Kusababisha umasikini kwenye jamii, vijana wanao tumia Madawa ya kulevya, huwa ni wavivu hawafanyi kazi halali za kuwaingizia kipato zitakazo wasaidia familia .
iv) Vijana wa rika dogo umri kati ya (13-18) kuuanza mapema kutumia Madawa ya kulevya na hivyo kuatarisha maendeleo chanya Kwa vijana hao mfano maendeleo ya elimu pamoja ,afya , kiuchumi.
Njia zitakazo tumika kuzui Biashara hii isiendelee kufanyika kwenye maeneo ya jamii.
I) Serikali kupitia wadau mbalimbali wa maendeleo kuendelea kuboresha maeneo ya masoko na minada kuwa ya kisasa, hii itasaidia vijana wa hovyo kushindwa kukaa kwenye maeneo hayo.
ii) Serikali kuendelea kuelikisha jamii juu ya athari za matumizi ya Madawa ya kulevya, kwenye maeneo mbalimbali ya jamii yetu hususani masokoni, minadani, kata.
iii) Mizigo inayosafirishwa kwenye mabasi ikaguliwe na idara husika.
iv) Taasisi husika, ziwe na utaratibu wa kuwabadilisha wafanyakazi wa kwenye hizo Taasisi zinazo pambana na Madawa ya kulevya, wasifanye Kazi Kwa kipindi Cha miaka 5 , itasaidia wafanyakazi kutoshawishika kufanya ulaghai kutoka Kwa walanguzi wakubwa.
Maoni:
Serikali makini na yenye viongozi waadilifu, Ndio itakayo weza pambana na walanguzi wa Madawa ya kulevya.