Mkutano wa CWT, Dodoma: Rais Magufuli awajaza pesa Walimu! Awataka kutochagua mtu kwa matakwa ya rushwa au siasa

Roving Journalist

JF Roving Journalist
Apr 18, 2017
3,540
13,214
Habari,

Leo ni ufunguzi wa Mkutano mkuu wa chama cha Walimu Tanzania unaofanyika Chimwaga Dodoma. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania amehudhuria .

walimu.PNG


Mkutano huu ni mara ya kwanza kwa mkuu wa nchi kukutana na walimu tangu kuchaguliwa kwake kushika madaraka katika serikali ya awamu ya tano

Mwenyekiti wa Chama cha Walimu Mkoa wa Dodoma, Augustine Njamasi amesema jambo kubwa ambalo walimu wanataka kuzungumza mbele ya rais Magufuli ni kutoa kilio chao cha miaka mingi cha walimu kutopata stahiki zao kwa wakati licha ya kuwa kada hiyo imekuwa kimya sana na hajaweza kuchukua maamuzi magumu.

“Kitendo cha kuwepo kwa rais katika mkutano huo mkuu wa walimu utazaa matunda kwani yatapatikana majibu sahihi na kwa wakati tofauti na miaka mingine ambayo walimu wamekuwa hawajui hatima ya madai yao ni lini yatalipwa,” amesema.

Mkutano hu utafanyika kuanzia leo Desemba 14 hadi 16 mwaka huu huku wajumbe wa mkutano wanatarajiwa kuwa na idadi ya wajumbe 3000 ambao wamehudhuri mkutano huu ambao ni wa Kikatiba.

Wageni waarikwa ambao walitegemewa kuambatana na rais ni Makamu wa Rais, Waziri Mkuu, makatibu wakuu wa Wizara mbalimbali pamoja na mawaziri.

Nitawapa kila kinachojiri kutoka ukumbini.

Karibuni

=====

UPDATES:





Msafara wa Rais Magufuli umeshawasili Ukumbini. Waziri Mkuu Pia kashafika akitokea Dar Es Salaam alipokuwa akiaga Miili ya Wanajeshi 14 waliofariki Vitani huko Congo.

Changamoto walizotoa walimu wanazokumbana nazo;

1. Posho ya kufundishia yaani teaching allowance.
walimu wanatumia muda mwingi sana kuliko watumishi wengine ambao muda wao ukiisha wanaondoka ofisini. Walimu wanabaki kuandaa vipindi vya kesho na wanashinda na wanafunzi wa boarding. Chama cha walimu kinapendekeza Serikali kurudisha Posho hiyo maana Mishahara ya walimu ni midogo na makato ni makubwa

2. Ujenzi wa nyumba za walimu
Kuna upungufu wa nyumba 100,960. Pia wameona jitahada mbalimbali zinavyofanywa na serikali juu ya hilo hasa mkoa wa Dar es Salaam

Hotuba ya Rais John Pombe Magufuli

Awali ya yote ndugu zangu napenda niwashukuru sana kwangu leo ni siku tofauti sana kwenye maisha yangu. Ndio maana mliponialika nilifurahi sana na nilipozungumza na mwalimu Kassimu Majaliwa tukasema lazima tuende wote. Mimi ni Mwalimu sijabadilika na shida na raha za uwalimu najua. Nafahamu raha ya kufundisha, mateso na machungu walimu wanayoyapata

Niungane nanyi kutoa pole kwa aliyekuwa Katibu Mkuu wa chama cha walimu, pia naomba kuungana nanyi kuwapa na kuungana na watanzaia wote kutoa pole marehemu wetu wanajeshi waliokufa wakilinda amani Congo na leo ilikwa siku ya kuwaaga. Pia tuwaombee wapone haraka majeruhi wetu

Waalimu mmefanya kazi kubwa sana, asanteni sana

Kwa lengo la kuendeleza mafanikio haya sisi tunachukua hatua mbalimbali ili kuboresha elimu yetu, tumeanzisha elimu bila malipo ikiwa tulitenga billion 18.77 na ilipofika julai 2016 tuliongeza hadi billioni 23.868. Hivyo kuanzia disemba 2015 hadi novemba 2017 tumetumia bilioni 535 kwa mpango wa elimu bure

Pia tumefanya marekebisho kwa shule 365 ikiwa shule kwonge ni 88. Marekebisho hayo ya miundombinu yalijumuisha nyumba 12, madarasa 1435, mabweni 261, majengo ya utawala 11 na miundombinu mingine

Pia tumeongeza mikopo kwa wanafunzi wa elimu ya juu kutoka billioni 373 hadi billioni 483 na wanafunzi wasomao ualimu zaidi ya 28 elfu wananufaika na mikopo hiyo

Pia umeongeza ruzuku kwa mashule kwa ajili ya posho za walimu wakuu na watawala wengine.

Mmesema mnadai billioni 25, shida tuliyokuwa twapana ni uhakiki. Mimi ni mwalimu mwenzenu kama mnavyosahihisha kwa usahihi na kuweka sifuri kwa wanafunzi wanaostahili mimi ndivyo nafanya kazi hivyo kwa uhakiki. Hivyo nina uhakika kwa mwalimu yeyeto angepewa nafasi yangu au ya Waziri Mkuu au nafasi yoyote asingekubali hayo

Ukienda kwa mfano kwenye TASAF kulikuwa na kaya masikini 56 elfu, mbejeo ambazo zinadaiwa ambazo ni hewa zaidi ya billioni 58

Kila nilipokuwa nagusa kulikuwa na mambo hewa kwenye Kandarasi kuna hewa, kwa walimu kuna hewa. Inawezekana hata kulikuwa na mapenzi hewa

Mimi ni mwalimu mwenzenu lifundisha hesabu na kemia hivyo kukrem naweza

Kama nilivyosema mimi ni mwalimu mwenzenu, na changamoto zenu nazijua. Hata mke wangu ni mwalimu na huwa anaikumbusha matatizo ya walimu [tena huwa anajua muda mzuri wa kunikumbusha] simahanishi hivyo, huwa ananikumbusha muda wa chakula

Nimefundisha Lugalo, Tosamaganga, Mwanza secondary baadae nikaenda Sengerema sekondari. Najua ugumu wa ualimu. Nashukuru mmeongea vizuri kuwa mnadai billioni 25 na zaidi. Palishawahi kuzungumza mtu mmoja aliyejifanya ni muwakilishi wenu bahati nzuri sasa sio mwalimu alisema mnadai zaidi ya trioni moja

Mkuulizwa bank ya walimu ambayo hata haifanyi vizuri, pengine ikafutwa na inatoa mkopo kwa watu ambao hata hawajui kushika chaki. Mnajua kudai ya serikali ila nyie pia mmnaibiwa hamuulizi. Nikiuliza zile 2% anazokatwa kila mwalimu zinaenda wapi nina uhakika walimu wenzangu hamjui.

Nilialikwa hapa kuenda kufungua bank ya walimu na nilitamani sana. Nilipopewa taarifa na BOT nilisikitika sana. Tanzania tuna bank 58 ila katika bank ambazo zinaweza kufutwa na kufilisika yenu ni moja wapo. Kwanini msiulize fedha mlizoweka ziko wapi, wale mliowaweka pale wanafanya nini?

Mwalimu J.K Nyerere alisema kuwa "Ndama hunyonya kiasi cha maziwa ambacho mama yake anacho" hivyo naomba mpokee kidogo tuwapacho walimu

Kazi ya ualimu nilipenda kwa sababu wanafunzi wakifunga na wewe unafunga. Ukihesabu hizi fungafunga ni nyingi kuliko waajiriwa wengine yote lakini mshahara hausimami. Mimi nlianza na mshahara wa 1453 nikiwa Sengerema sekondari na baadhi ya wabunge niliofundisha ni Nkamia na Lugola, ambaye alikuwa kiranja wa bweni la Mirambo. Sasa walimu tuvumiliane tu posho hiyo itarudishwa endapo mambo yatakaa vizuri

Watu wanasema vyuma vimekaza, weka grease na hawa wanaosema hivi ni wale waliozoea vitu vya hewa. Walimu hewa wafanyakazi hewa na wengine. Hawa vyuma havitakaza tu na vitavunjika kabisa

Niawaombe sana walimu, msije kuchagua watu kwa matakwa ya siasa, msikubali pia kuchagua viongozi kwa rushwa. Mimi kwenye chama changu cha CCM hata kama watu watabaki watatu sitajali lakini mtu yoyote akitoa rushwa atakamatwa, na tumewakamata wengi na wengine hatuwasemi tu.

Kuna mmoja tulimtegea mtego huko Singida kwenye guest moja hivi ametukimbia ana bahati yake, najua kwenye kikao hiki hayupo ila ujumbe umfikie, mara nyingi anajifanya msemaji wa chama cha walimu.

Siku hizi kuna sheria ya takwimu, ukizungumza tu takwimu za uongo kwa lengo la kutaka kupata umaarufu sisi tutashughulika na wewe

Najua walimu mmetoka mbali, mmliohudhuria hapa ni 1200, hivyo nachangia millioni 10 kwa ajili ya chakula cha mchana. Lakini Millioni 10 ndogo kwa walimu wote hawa. Mhe. Waziri Mkuu nawe ongeza hapa. Rais awataka mawaziri nao kutoa ahadi

Waziri Mkuu, Kassimu Majaliwa - Millioni 10
Waziri Prof. Joyce Ndalichako - Millioni 6
Waziri Jenesta Mhagama - millioni 6
Mwalimu Dkt. Filapo - Millioni 4
Mke wa rais Mama Janeth Magufuli - Millioni 1
Mke wa Waziri Mkuu mama Majaliwa - Millioni 1
Spika wa Bunge, Job Ndugai - Millioni 5
Naibu katibu Mkuu TAMISEMI, Nzunda - Millioni 4
Prof Mwamfupe, Mstahiki Meya wa Dodoma - Millioni 1
Mkuu wa mkoa Dodoma, Dkt. Bilinith Mahenge - Millioni 2
Waziri Prof. Juma Mkuchika - Millioni 3
Mkuu wa chuo cha Dodoma, Prof. Idriss Kikula - Millioni 4
Mkurugenzi wa Usalama, Kapilimba - Millioni 3

Jumla ya kiasi cha fedha kilichokusanywa ni Millioni 60
 
Unafki tu.
Mawalimu hayajielewi kabisa.Hayajawekewa increments zao na madai yao halafu yanafurahia hapo.

Et 6600 ndo ongezeko kama sio dharau hiyo ni nn?

Watanzania daini katiba mpya na tume huru ccm itoke vinginevyo mtapata tabu sana.
 
Back
Top Bottom