KWELI Matumizi ya vyombo vya plastiki kuwekea chakula au vinywaji vyenye joto kali yana madhara kwa binadamu

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Katika jamii yetu ya kitanzania asilimia kubwa inatumia vyombo vya plastiki kunywea na kulia chakula, lakini nimekuwa nikisikia kuwa plastiki ina madhara makubwa kwa afya ya binadamu, wapo wanaodai inasababisha saratani, wengine inamaliza nguvu za kiume kwa wanaume na mambo mengi.

Je, ni kweli ina madhara? Maana napata mashaka kwani sijawahi kusikia serikali ikisema kuhusu madhara hayo au kukemea matumizi yake wala kutoa elimu ya namna ya kuvitumia.

1716343583310.jpeg

 
Tunachokijua
Plastiki ni aina ya maunzi mango yanayoundwa kwa njia ya kikemia na kukubali umbo lolote yakiwa teke.

images
Ni jambo la kawaida katika jamii kutumia vyombo vya plastiki katika shughuli mbalimbali kwenye maisha ya kila siku licha ya kuwepo sintofahamu ya usalama kiafya juu ya matumizi ya vyombo hivyo hivyo kama kweli ni salama au lah.

Je, ni kweli vyombo vya plastiki vina madhara?

JamiiCheck
imepitia machapisho mbalimbali na kubaini kuwa ni kweli matumizi ya vyombo vya plastiki kwenye kuwekea chakula tunachokula, kunywa yana madhara iwapo matumizi hayo yasipokuwa sahihi. Matumizi sahihi ni kuhakikisha chombo husika kinatumiwa pasipo kuwekwa kwenye moto au joto kali.

Unaweza kutumia kikombe cha plastiki kunywea maji ya baridi, lakini ni hatari kukiweka chombo cha plastiki kwenye oveni au kuweka vitu vyenye joto kali kama chai. Plastiki ikiwa karibu na moto au joto kali huyeyuka na kutoa chembechembe ndogo ambazo ama unaweza kuzinywa na maji au kuzila pamoja na chakula na kusababisha madhara kiafya, baadhi ya madhara hayo ni kupata saratani na magonjwa mengine kama ya afya ya uzazi.

bec1b68122897f30455957ceb1cd3bdfa0484298.jpeg
Usitumie kabisa vyombo vya plastiki kuchemshia au kuwekea vyakula vya moto kama chai, maziwa, supu, maji, ugali nk. Hii ni kwa sababu plastiki inapopata moto, huzalisha kemikali iitwayo BPA (Bisphenol A) ambayo ikiingia mwilini husababisha magonjwa mengi kwa binadamu.

Plastiki zina matumizi makubwa lakini pia zina athari kwenye afya yetu, ni vyema ukatumia vyombo vya udongo, kioo kwa maana ya glasi au mbao badala ya plastiki iwapo utakula au kunywa vitu vyenye joto kali. Madhara ya plastiki huonekana muda mrefu baada ya kutumia.

Chapisho liliandikwa na Harvard Health Publishing linasema: Uchunguzi umegundua kuwa kemikali fulani kwenye plastiki zinaweza kutoka nje ya plastiki na kuingia kwenye chakula na vinywaji tunavyokula. Baadhi ya kemikali hizi zimehusishwa na matatizo ya kiafya kama vile matatizo ya kimetaboliki (pamoja na unene uliokithiri) na kupungua kwa uzazi. Usafishaji huu unaweza kutokea kwa kasi zaidi na kwa kiwango kikubwa wakati plastiki inakabiliwa na joto.

1716341958327-png.2996430

Afya za watanzania zinachezewa sana. Unakuta mtu anafungiwa mihogo ya moto kwenye kifungashio cha nylon.

Imefika pahali hadi supu inafungashwa kwenye nylon.

Pia naomba wataalamu mtuambie kama foili nayo ina madhara. Maana matumizi yake yamekithiri hasa kwenye kufungasha kiepe (chips). Isije ikawa ndio moja ya sababu ya kupelekea upungufu wa nguvu za kiume.
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom