Webabu
JF-Expert Member
- Apr 29, 2010
- 7,448
- 11,415
Tatizo kubwa linaloikabili Ukraine kwa sasa ni kukosekana kwa nguvu kazi ya kuendeleza vita. Hilo linafuatiwa na upungufu mkubwa wa silaha.
Pamoja na kuzuiwa watu wenye umri wa miaka 18-60 kutoka nje ya nchi lakini zaidi ya watu milioni 4 wamekimbia nchi kwa kuvuka mto.
Ukraine imejaribu kubadili sheria ili walioko nje warudi nchini kwa lazima wapate kusajiliwa jeshini,kwa mfano kila mwenye paspoti ya Ukraine haruhusiwi kuibadilisha kwenye balozi za nchi hiyo za nchi waliko,ni lazima warudi nchini.
Kwa kujua madhumuni ya sheria hiyo walio nje wanajibu jeruri kusema hawaoni sababu ya kurudi huko,ni bora kuchukua uraia wa nchi nyengine kuliko kurudi nchini ambako hakuna matumaini ya kushinda vita.
Hali inayoikabili Ukraine haihitaji nyongeza ya silaha wala fedha,muhimu ni askari wa kutumia hizo zana ambazo nazo kila nchi kati ya marafiki wa Ukraine ameshachangia na kukata tamaa.
Marekani imeidhinisha kiasi kikubwa cha fedha kwa Ukraine,takribani dola bilioni 62.Hata hivyo msaad huo ni wa kijanja na kiasia kwani hautotolewa papo kwa papo na wala hautoshikwa mkononi mwa Ukraine mpaka muda mrefu upite huku Urusi ikizidi kusonga mbele kuelekea Kyiv au pale watakapoamua kusimama.
Msaada iliyotoa Marekani ni mdogo kuliko iliyokwishokutolewa huko nyuma na ambayo haikuleta tija yoyote.
Msaadu uliotolewa safari hii utakuwa ni kwa awamu kwa kutoa fedha hizo kwenye makampuni ya utengenezaji silaha ya ndani ya Marekani ili watengeneze silaha zitakazofidia kurudisha silaha zilizotolewa kwenye maghala kuipatia Ukraine.
Silaha kama hizo kutoka kwenye maghala muda mwengine zinakuwa zimepitwa na wakati na zikiingia uwanja wa mapambano huwa hazifanyi kazi kisawasawa.Hilo limetokea mara nyingi kwa silaha kutoka Ujerumani na nchi nyengine za jumuiya ya NATO ambapo Ukraine imekuwa badala ya kutoa shukran kwa misaada hiyo imewatolea kashfa waliowapatia silaha hizo kwa kutangaza hadharani kuwa ni mbovu.
Ukipenda unaweza kuongeza maarifa kuhusu tatizo la Ukraine hapo chini.