watanzania nipeni kazi

rosemarie

JF-Expert Member
Mar 22, 2011
6,887
3,412
natamani kurudi nyumbani
mimi sio mfanya biashara,nimekuwa nikifanya kazi sehemu mbalimbali hapa africa kusini
nimejifunza mambo mengi sana ambayo natamani niyatumie nyumbani,
nitarudi kama mtanipa kazi serikalini hasa kwenye idara ya mambo ya ndani kitengo cha passport,
kwa mtazamo wangu watu wanaofanya kazi hapo idara ya passport hawajasafiri,hawajui nini maana ya halisi ya kitabu kiitwacho passport,
waziri unayehusika nipo tayari kuja kushirikiana na nyie hapo nyumbani tufanye kazi pamoja na kudhibiti kabisa huo mpango unaendelea hapo sasa hivi wa kuwapa passport raia wasio watanzania,
watu wengi wasio raia wa tanzania wanachukua passport kirahisi sana kwa sababu ya watoaji waliopewa mamlaka hawajui wanachokifanya,
narudia tena nipo tayari kuja nyumbani tu-form proccess mpya ya kudhibiti kabisa passport zetu kushushwa thamani.kama africa kusini na botswana na nchi nyingi za kiafrica wameweza kudhiti hata sisi tunaweza,
nitatoa email zangu na no zangu za simu kama kuna aliye tayari kwa hili,
 
thabo, hongera kwa moyo wako wa ujasiri wa kutaka kurudi nyumbani na kurekebisha mambo. ila naungana na husninyo, huwezi pata hata mke kwa mkwala. kuna utaratibu wa kupata ajira serikalini (unless una memo nzito nzito nazo haziji kwa mikwala,lol). uwe unapitia website ya utumishi na mitandao ya job adverts na uombe kazi kama watu wengine, achana na mkwala wa kuwa kama unahitajika wakutafute sijui nini. kila la kheri
 
husninyo nia yangu ni kuja kutoa mchango wangu kwenye hilokama wakikataa basi naendelea na maisha kama kawaida!
nia yako ni nzuri ila utafanya mambo kinyume na wao na wao wanaelewa wanachokifanya sio kizuri ila wana maslahi binafsi. Hiyo nia ingebidi uioneshe wakati upo ndani ya system tayari. Kibongo bongo kwanza ukienda kuomba kazi sehemu kama umemzidi bosi wako kisomo unabaniwa.
 
thabo, hongera kwa moyo wako wa ujasiri wa kutaka kurudi nyumbani na kurekebisha mambo. ila naungana na husninyo, huwezi pata hata mke kwa mkwala. kuna utaratibu wa kupata ajira serikalini (unless una memo nzito nzito nazo haziji kwa mikwala,lol). uwe unapitia website ya utumishi na mitandao ya job adverts na uombe kazi kama watu wengine, achana na mkwala wa kuwa kama unahitajika wakutafute sijui nini. kila la kheri

king"asti ngoja nikupe siri,
ukitumia website kamwe hawajibu,nilijaribu kuongea na waziri wa mambo ya nje na secretary aliniahidi kuwa atafikisha ujumbe,
cha kushangaza mpaka leo ni mwaka hamna majibu,nimendika email nyingi hamna majibu.
nimeweka hapa kwa ssababu wahusika wapo hapa na wanasoma hizi topic
nimesema ninajitolea kuja tufanye kazi pamoja,thats all
ningependa iwe hivyo.
 
Unataka Kazi bila ya mshahara au unatafuta Kazi Wzara ya Mambo ya Ndani?
 
Unataka Kazi bila ya mshahara au unatafuta Kazi Wzara ya Mambo ya Ndani?

nitafanya kazi ya kujitolea bila mshahara kwa miezi 6
baada ya hapo wakipenda wanaweza kuniajiri,lakini katika hiyo miezi 6 tutahakikisha tunarekebisha kabisa mfumo mzima na ndio utakuwa mwanzo wa safari ndefu ya system mpya,naamini hili litakuwa jibu la ahayo matratizo
 
Nafikiri umekaa mno huko na kuisahau tanzania,huku mkono mtupu haulambwi!
 
Mijitu mingine bwana, watu wana apply kazi JF? siu apply huko wizara ya mambo ya ndani? vipi kijana?
 
nitafanya kazi ya kujitolea bila mshahara kwa miezi 6
baada ya hapo wakipenda wanaweza kuniajiri,lakini katika hiyo miezi 6 tutahakikisha tunarekebisha kabisa mfumo mzima na ndio utakuwa mwanzo wa safari ndefu ya system mpya,naamini hili litakuwa jibu la ahayo matratizo
Kama ni kweli nataka nijue motivation yako nini? Baada ya mabadiliko unataka waseme "XXX" ndio aliokoa migration department ya TZ? Ao unataka nini hasa? maana hakuna mtu anaweza kufanya kazi bila personnal motivation. Na please usiseme ni sababu unaipenda inchi yako coz tunaipenda sote.
 
Mijitu mingine bwana, watu wana apply kazi JF? siu apply huko wizara ya mambo ya ndani? vipi kijana?

nafikiri watu kama hawa wanashusha heshima ya jf,mzee ukisoma post jaribu kafikiri kabla ya kujibu
 
Kama ni kweli nataka nijue motivation yako nini? Baada ya mabadiliko unataka waseme "XXX" ndio aliokoa migration department ya TZ? Ao unataka nini hasa? maana hakuna mtu anaweza kufanya kazi bila personnal motivation. Na please usiseme ni sababu unaipenda inchi yako coz tunaipenda sote.

hello Roulette
nitaongea ukweli kutoka moyoni,
nasikitika sana kuona watu wa mataifa mbalimbali wengi wakija hapa south africa kwa kutumia passport za tanzania,
motivation yangu kubwa ni kurudisha heshima ya taifa
nataka na mimi nijitolee nifanye kitu ambacho kinaweza kuleta mabadiliko katika mfuma mzima wa utoaji vitabu vya passport,
sitaki mseme nilifanya hii kazi wala sitafuti umaarufu
nataka nitoe mchango wangu kwenye system mbovu kabisa kuliko yote duniani
 
Vacancies
[h=1]Ministry of Home Affairs Website[/h]

We regret we do not have vacancies at the moment

TRY TO INQUIRE ANY VACANCY THROUGH FOLLOWING ADDRESSES:

Permanent Secretary
Ministry of Home Affairs
P.O. Box 9223, DAR ES SALAAM
Tel No: +255 - 22- 2119050
+255 - 22- 2112036
+255 - 22- 2112040
Fax:+255 - 22- 2119050
E-mail: ps@moha.go.tz This e-mail address is being protected from spambots, you need JavaScript enabled to view it
Principal Commissioner of Immigration
P.O. Box 512 DAR ES SALAAM
Physical location:Loliondo Street Kurasini
Tel :022211218
Utawala: admini@immigration.go.tz This e-mail address is being protected from spambots, you need JavaScript enabled to view it
Ubalozi: consular@immigration.go.tz This e-mail address is being protected from spambots, you need JavaScript enabled to view it
Mafunzo: training@immigration.go.tz This e-mail address is being protected from spambots, you need JavaScript enabled to view it
Sheria: legal@immigration.go.tz This e-mail address is being protected from spambots, you need JavaScript enabled to view it
Uwanja wa Ndege wa JNIA:
jkn_airport@immigration.go.tz This e-mail address is being protected from spambots, you need JavaScript enabled to view it
Public Relations/general:
info@immigration.go.tz This e-mail address is being protected from spambots, you need JavaScript enabled to view it Email: Tovuti:Ministry of Home Affairs Website

thabo, ni vizuri kuwa na nia nzuri uliyonayo. ili kuelewa kuwa walioko nyumbani sio wote hawana nia na ujuzi wa kufanya vizuri, inabidi uingie kwenye system. katika kukuandaa tu kiasikolojia, dont expect any special treatments kama mtanzania mwenye ujuzi na uliyeupata nje ya nchi. nobody cares! na huyo balozi uliyeongea nae i am sure kabla hujaondoka mbele ya uso wake alikuwa tayari keshasahau ulichoongea nae (pengine atakumbuka viatu vyako kama vilikuwa eye catching!! hayuko interested sana na changes unless otherwise stated) Angalia posts zinazotangazwa na uombe kazi ile tu iliyotangazwa. i find it working better kupata chance and then ukaonesha umahiri wako ukiwa ndani kwa kutoa mawazo pale unapopata wasaa. sitojali kama utapata umaarufu woote uliopo duniani kwa kuleta mabadiliko manake utayastahili. ninachoongelea ni kuwa kuna taratibu za kupata ajira mahali popote serikalini. otherwise waandikie watu kama radar na recruitment agencies na uwaambie interest yako ni immigration tu, wakipata chance watakuita uka-compete na wengine

thank you ngoshwe,nitawasiliana nao na kuwapa proposal yangu tuone itakuwaje

nia yako ni nzuri ila utafanya mambo kinyume na wao na wao wanaelewa wanachokifanya sio kizuri ila wana maslahi binafsi. Hiyo nia ingebidi uioneshe wakati upo ndani ya system tayari. Kibongo bongo kwanza ukienda kuomba kazi sehemu kama umemzidi bosi wako kisomo unabaniwa.
 
Wazo ni zuri ila kibongo bongo sikushauri, yaani unataka kutibua dili za watu? watakuua kabla ya muda wako.

Mwa.Nyerere alijaribu kuzuia ufisadi akadungwa sindano ya sumu iliyomuua tartiibu.

Hii nchi ina wenyewe, ukileta uzalendo wanakuulia mbali.Watch out.
 
ok then!
ngoja niendeleze maisha yangu hapa na kusahau ya huko,
hapa naishi vizuri sana lakini kelele za nchi yangu haziishi masikioni mwangu,nitajifunza kuziba masikio yangu na kuendeleza maisha yangu kama kawaida,
kwa taarifa ni kwamba hiyo nchi haina mwenyewe,kwa herini!,..
 
Back
Top Bottom