Ufugaji wa kisasa wa Nyuki: Faida, Utaalam na Masoko

misorgenes

JF-Expert Member
Oct 7, 2010
206
50
Anayejua elimu/ujuzi wa ufugaji wa Nyuki, Mizinga bora,ulinaji asali na soko la asali atupe elimu. Natamani kufanya biashara hii.

1.jpg

===========
Ericus Kimasha

..1. Naomba ufafanuzi nasikia kuna asali nzito na nyepesi, pia asali ya nyuki wadogo na asali ya nyuki wakubwa. Kuna Asali ya aina gani na ipi?

Ni kweli ziko asali nzito na nyepesi, amber, nyeupe na nyeusi. Uzito au rangi za asali kwa kiwango kikubwa huchangiwa na aina ya maua ambayo nyuki huchukua mchozo wa kutengenezea asali. Mfano asali ya maeneo mengi ya Tabora ni nyeusi wakati ile ya Singida maeneo ya Sanjaranda na Itigi ni amber ilhali ile ya Dodoma ni nyeupe na ina machicha kama barafu.

Aina ya nyuki wanaofungwa zaidi katika maeneo ya Kitropiki na Tanzania ikiwemo ni Apis Mellifera mbao tuliowengi tunawafahamu kama nyuki wakubwa. Hawa nyuki ni wakali na wana mwiba unaotumika kujihami. Tofauti na nyuki wadogo ambao ni wapole na asali yake inatumika zaidi kama dawa

..2. Je, ufugaji wa nyuki una msimu? Miezi ipi basi ni mizuri kwa Ufugaji wa Nyuki?
Ufugaji wa Nyuki ni kazi ya kudumu lakini uvunaji wa mazao ya nyuki hufanyika kwa misimu. Iko mikoa nchini mwetu ambayo huwa na misimu miwili kwa mwaka; Msimu mdogo na msimu mkubwa. Maranyingi asali inayopatikana katika msimu mdogo huwa ni ya masega ambayo hayajakomaa. Ninaweza kukushauri kwenye hili pale utakapo kuwa umeisha amua wapi utaweka mizinga. La muhimu ni kujua msimu wa maua unaanza lini. Hii itakusaidia kupata nyuki-wakaaji hii itakuhakikishia masega kujenjwa katika muda mfupi.

..3. Asali nzuri inayopendwa sana ni ya mkoa gani?
Watanzania wengi wanapenda asali ya amber. Ili kisayansi asali ya Dark-Blue ina virutubisho vingi zaidi. Mkoa wa Kigoma unaibuka kama chanzo cha asali nzuri na bora. Ninaposema bora namaanisha ulinaji unaozingatia kanuni bora, ukamuaji unaojali usafi na upakiaji katika vifaa safi na bila kuongeza kitu chochote (adulteration)

..4. Utengenezaji wa mizinga unakuwaje, ukubwa wa mizinga au dimensions ipi ni kikomo au ipi ni safi? gharama za kutengeneza mzinga ni ipi?
Iko mizinga ya aina mbalimbali na hivyo bei tofauti tofauti. Kwa maelezo ya kina nitumie email ekimasha@jamiiforums.com

..5. Utoaji wa asali unakuwaje lita ngapi kwa dimension ipi ya mzinga?
Aina ya mzinga inaushawishi katika ubora na kiwango cha asali inayopatikana. Majibu zaidi ya swali hili nitayaandaa au nitakupatia vitabu vyenye vipimo ambavyo vitakupanua uelewa kwenye suala hili.

..6. Mahitaji muhimu kwa ufugaji wa nyuki / kinachovuta nyuki ni kipi?
Miti na maua yanayotoa mchozo ni muhimu sana. Lakini pia chanzo cha maji lazima kipatikane katika eneo la mzingo usiozidi ekari tano

..7. Asali inaiva inakomaa baada ya muda gani?
Sikumbuki vizuri. Nitauliza

..8. Soko la Asali kwa bei ya jumla lipo wapi hapa dar?
Soko la Jumla litakulipa lakini si vizuri sana kama kupaki kwenye chupa na kusambaza katika Min and Supermarkets. Pia unaweza kufanya direct home delivery. Soko la Jumla liko kwa wapakiaji wa Dar (Honey Packers) ambao wengine hufuata moja kwa moja kutoka huko mikoani.

..9. Je soko la nje la asali lipo wapi sana? Usafirishaji wa Asali nje ya nchi unakuwaje?
Mimi ni muumini wa soko la ndani. Hii inatokana na ugumu na vikwazo vingi vilivyoko katika soko la nje na mwisho wa siku profit-margin ni ndogo sana. Soko la ndani ni kubwa mno ndo maana bado supermarkets zetu zimejazwa na asali kutoka Brazil, india na China.
 
Habari mkuu,nenda pale LITI- Morogoro wana kitengo cha ushauri utajifunza mengi. Au for practical guide fika maili moja Kibaha mkoani karibu na Polisi kuna msitu wanafuga kisasa.
 
Dah afadhali umeamua kuanza harakati za kijiajiri mapema. Na mimi nataka kujiajiri nitafurahi kupata maelekezo juu ya ufugaji nyuki
 
Nakushauri project yako ianzie Tabora, kule kuna mapori safi kwa ufugaji wa nyuki.

Nakumbuka nilifanya project hii na babu yangu nikiwa primary, sikuipenda sababu lazima ujue kutengeneza nyumba ya nyuki (mzinga)
Kutafuta sehemu nzuri juu ya mti na kuupachika (lazima ujue kukwea miti)

Kilichonifanya nichane na hii project ni ile siku la kurina asali, hatukuwa na protective clothes, tulikoka moto moshi wake ndiyo ulitumika kuwazuia nyuki wasituume, mzee nikabandikwa na nyuki 2 duh, ni mbio home na toka siku hiyo nikaiacha kazi hiyo rasmi.

Jaribu pia kufanya upembuzi wa hili suala la ukusanyaji wa Bee Products yaani NTA na Asali katika mikoa hiyo, inalipa naona MO pia anafanya hizo katika ukanda huo.
 
Nadhani the best way to tackle hii issue ni kuangalia from selling point of view, market.... Je unaweza kununua asali lets say from Tabora ukaipackage vizuri na kuiza nchi za nje au sehemu nyingine.

From my research other people make more money from bees than the bee keepers just like the middle men wanavyotengeneza pesa zaidi kuliko wakulima wenyewe. Kwahiyo soma hiyo link niliyokupa hapo juu kuhusu kufuga nyuki ila kama unataka kama biashara pekee utatengeneza more money kuinunua kwa jumla from tabora (including nta) package vizuri na kuresale kwenye supermarkets, au nchi nyingine

My point being to make profit from eggs you dont need kufuga kuku unless you love and you are ready kufuga kuku na kuna forum ya wafuga nyuki Can you make a living with Bees - Beesource Beekeeping Forums
 
nakushauri project yako ianzie Tabora, kule kuna mapori safi kwa ufugaji wa nyuki.

Nakumbuka nilifanya project hii na babu yangu nikiwa primary, sikuipenda sababu lazima ujue kutengeneza nyumba ya nyuki (mzinga)
Kutafuta sehemu nzuri juu ya mti na kuupachika (lazima ujue kukwea miti)

vip kuhusu iringa? jamani? mana nimeona kama na penyew panafaa ivi!
 
Nakumbuka nilifanya project hii na babu yangu nikiwa primary, sikuipenda sababu lazima ujue kutengeneza nyumba ya nyuki (mzinga)
Kutafuta sehemu nzuri juu ya mti na kuupachika (lazima ujue kukwea miti)

vip kuhusu iringa? jamani? mana nimeona kama na penyew panafaa ivi!
Ndio sababu nimesema kwenye post ya 7 unaweza kutengeneza pesa from honey na nta bila kufuga nyuki, unanunua kutoka tabora unapackage vizuri alafu unaiuza sababu huu ufugaji ili ufanye in big way you need good management na je utapata good return on investment kulingana na bei utakayouza (competition) au is it easier ukinunua tabora ambapo supply ni kubwa?

Je demand ni kubwa sana au utatafuta soko nje ya nchi? je kupata soko nje ya nchi ni lazima wewe ufuge au unaweza ukapata from tabora package na ukaaza nje na kubakia na profit nzuri? haya ni baadhi ya maswali ya kujiuliza.
 
voiceofreason: ngoja nifanye tafiti za kina! mana bado nipo kweny steji za kwanza kabisa!
 
Anza na kuuza bee products,then uingie ktk ufugaji,kwani kwa sasa wafugaji ni wengi,ila Distributors ni wachache mno na benefits za nyuki na Asali bado jamii yetu bado haijaitambua ipasavyo
 
nakushauri project yako ianzie Tabora, kule kuna mapori safi kwa ufugaji wa nyuki.

Nakumbuka nilifanya project hii na babu yangu nikiwa primary, sikuipenda sababu lazima ujue kutengeneza nyumba ya nyuki (mzinga)
Kutafuta sehemu nzuri juu ya mti na kuupachika (lazima ujue kukwea miti)

vip kuhusu iringa? jamani? mana nimeona kama na penyew panafaa ivi!

Ndio Iringa ni pazuri, nimefanya ziara ktk vijiji fulani Iringa,yaani kuna nyuki balaa. Wilaya ya Kilolo ina misitu ya kiasili mizuri ya kufugia nyuki
ktk kijiji cha Itimbo,ni km 39 toka Iringa mjini. Ukienda Image/Lyasa huko kuna nyuki wengi na miti ya kiasili mingi tu. Dabaga vegetable wa Iringa wanasindika asali pia, you can go for more details.

Bahati mbaya watu wote wanaijua Tabora,lakini Chunya ni potential zaidi kwa ufugaji wa nyuki wadogo ambao ni dili zaidi. Tatizo lake nyuki wadogo hawatoi asali nyingi kama nyuki wakubwa.
 
lets be partners then!

Mkiunganisha nguvu mtafanikiwa haraka, kwa mfano,mwezi jana nilipokuwa kijiji kimoja kinaitwa Chogo huko Iringa,niliona mzinga mmoja unafikia Tsh 8000/ kuutengeneza kisasa pale pale kijijini na wenyewe wanasema una ujazo wa debe moja na nusu. Mavuno ni mara mbili kwa mwaka.
 
Mimi nashauri, kama una maanisha ktk plan zako, anza na shamba lako ili uweze kudhibiti ubora wa asali yako. Mashamba ambayo yanazungukwa na mashamba ya mazao mengine yanayotumia dawa za kilimo ni hatari kwa ubora wa asali yako. Kumbuka nyuki anaweza kwenda umbali wa kilomita 4 toka ulipo mzinga wake, hivyo tafuta shamba zuri lililo karibu na maji safi ya kuaminika na lisiwe karibu na mashamba yanayotumia dawa za kuulia wadudu.

Kutembelea wakulima wakubwa ni muhimu sana kwa ajili ya practical,kabla hujaanza ili wakupe mawili matatu.
 
embu nieleze vizur iyo propolis!

Kazi nyingine ya propolis ni kuvutia nyuki ili waingie ktk mzinga mpya,yaani ukishapata mzinga mpya,nenda shambani kwako, fungua ndani ya mzinga kisha paka ktk kuta za mzinga hiyo propolis yako,funika na uondoke. Usifanyie nyumbani kwako,kwa sababu unaweza ukasahau kupeleka shamba na nyuki wakaingia mchana, watoto wako au wa jirani wakachezea. Balaa lake si dogo.
 
Naamini umepewa mawazo mazuri mengi tu.
Kwa kuongezea, napenda kukukumbusha kuwa ktk modern beekeeping techniques hulazimiki kwenda porini kama unavyoelezwa kuwa utafute sehem zenye misitu mikubwa ila andaa shamba lako kwa kupanda miti ambayo inatoa maua yanayopendwa na nyuki.
Congrats.
 

Similar Discussions

Back
Top Bottom