Nimebahatika kufanikiwa kupeleka vitu vya kufungua Hospitali Tanzania ambavyo nimevipata hapa USA kwa miaka miwili na nusu. Vitu vyote ni vya Hospitali na sijachanganya Container langu na kitu chochote ambacho sio cha hospitali. Nina List niliyopewa na barua zakuonyesha kuwa vitu ni vya misaada kwa Hospitali mpya ninayotaka kufungua. Sasa bandarini Tanzania watu wa TRA wanasema eti sio vitu vyote vina msamaha wa kodi na kusema vitu kama vitanda havina msamaha. Vitanda ambavyo ni vichache ninavyo ni vya Hospitali na ni vifaa vya kihospitali sio vitanda vya vyumbani, Dialysis Chair sio kitu cha nyumbani bali ni kiti cha kutumia wakati wa kufanya Dialysis. Sasa sisi tunahangaika huku kujaribu kusaidia kwa kufanya kazi usiku na mchana ili kufungua Clinics ambazo ukiangalia vizuri hatupati kitu lakini vikwazo visivyo vya msingi vimewekwa na TRA ili kupata sababu ya kuomba rushwa. Sasa huyo jamaa wa TRA anaomba rushwa kama nataka vitu hivyo vitoke vyote na mimi sitatoa rushwa kwa mtu yeyote. Vitu vyangu vikipigwa Mnada mimi na Tanzania basi! nilikuwa nataka kuleta CT Scan ambazo ni hadimu Tanzania lakini nikiendelea kusumbuliwa bila sababu ya msingi sitafanya hivyo tena na watakao umia ni Watanzania masikini. Raisi yuko New York anaomba misaada lakini sisi Watanzania wenzake tunaofanya jitihada za kusadia nchi na uchumi tumekuwa watu wa kunyanyaswa bila sababu za msingi. Kama Watanzania wanaofanya kwenye hizi sehemu hawana uzalendo je mnategemea vipi nchi yetu kuendelea. Je kama Tanzania itatukosa sisi ambao tumetumia pesa zetu, muda wetu kuleta vitu kama vya hospitali na kusumbuliwa je tutategemea wazungu watusaidie mpaka lini badala ya kujisaidia wenyewe. Kama nivyosema siku za nyuma kama hutuwezi kubadilika tusilalamike kwa umasikini.