Mapenzi yananitatiza

omwana

Member
Mar 2, 2010
46
0
Nawasalimu wana jamii, pia nawapa pole na mihangaiko ya hapa na pale

Pamoja na salaam pia naombeni ushauri. Naomba kwa yeyote aliyetayali kunishauri anishauri kwa dhati ya moyo wake, si kukejiei wala nini sababu hii siyo hadithi bali ni kitu cha ukweli na ndo maana nimeamua kuleta hapa mbele yenu muweze kunishauri kwani niko njia panda.

Niko katika mahusiano ambayo kwa kweli yananiacha njia panda, nina jamaa yangu wa muda mrefu tu, binafsi yangu nampenda sana huyu bwana, japo na yeye anaonyesha kunipenda lakini simuelewi sana. Mimi nina mtoto ambaye sikuzaa nae, huwa anaonyesha mapenzi makubwa sana kwa mtoto wangu ikiwa ni pamoja na kunisaidia kumlipia ada, kuongea nae kwenye cm kama vile baba afanyavyo kwa mtoto wake, akiwa nae anamtambulisha kwa marafiki zake kwamba ni mtoto wake wa kumzaa mimi pia ananiita mkewe, tunaishi mbali mbali (yaani mikoa tofauti) yeye yuko Dar mimi niko Mwanza. Tatizo liko kwenye kufunga ndoa, nimekuwa nikiwambia mara kwa mara kufunga ndoa lakini amekuwa akinipa moyo kila kukicha kwamba usiwe na haraka tutafunga tu ndoa, hili si jambo la kufanyia haraka na maneno mengine kibao, tumependana tangu mtoto wangu akiwa darasa la kwanza na hivi sasa mtoto yuko kidato cha tatu.

Nikiwa karibu nae kwa kweli namuonyesha mapenzi yangu ya dhati kwa kumpikia, kumfulia na kufanya vile ambavyo mke mwema anatakiwa kufanya. Ndugu zake kama dada, kaka na wadogo zake wananifahamu, wao pia wanipenda pamoja na mtoto wangu na wanasema sisi hatumtambui mtu mwingine zaidi yako.

Moyo wangu huko kwake, sijisikii kuwa na mtu mwingine kabisa ni kwamba nampenda sana, na yeye pia anaonyesha kunipenda, hila siwezi jua moyoni mwake. Sasa wapendwa wanajamii naombeni msaada wenu wa ushauri, kama wewe ni mwanamke nisaidie kama ingekuwa wewe ungefanyaje na kama ni mwanaume angalia hii hali na unishauri kwa kuwa wewe ni mwanamume na hii hali ya mwanaume mwenzio unaionaje? Naomba tusifanye kejeli wala utani.
 
mimi kitu cha kwanza ningefanya ni kuwa nae karibu....distance is something else
 
Upendo wa kweli angeubadilisha kuwa NDOA!

NINA MASHAKA NA HUKO KUKUPENDA KWAKE!

Miaka hiyo karibia 7 anakuzingua tu, huoni kuna mambo fulani inaendelea?

Tena ingekuwa bora hata mngekuwa mnakaa pamoja, at least ungekuwa na uhakika kwamba unammiliki, lakini yeye Dar, wewe Mwanza....%$&***#network searching!
 
mmmh pagumu kiasi......
mbona muda mrefu sana, kama mwapendana kweli basi ndoa inasubiri nini muda wote huo??
baba wa mwanao naye yuko wapi mpendwa??
 
Harambee: Saidia wahanga wa mafuriko Tanzania; zaidi ya watanzania 1960, wamechangia!
Mzee Mwanakijiji
user_offline.gif
8th January 2010, 09:34 PM
Agenda for Action:

harambeeredcross.jpg


SIKILIZA MAHOJIANO NA TANZANIA RED CROSS:



SIKILIZA PRESS CONFERENCE:



SIKILIZA Mahojiano na Clouds FM:



%5Craismtandaotaalumajan13.jpg


Rais wa mtandao wa wanataaluma Tanzania(TPN), santus Mtsimbe, akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es salaam jana, kuhusu TPN kwa kushirikiana na jamii Forum kukusanya Sh 10 bilioni za kuwasaidia waathirika wa mafuriko nchini. Picha na Michael Jamson.

Source: http://www.mwananchi.co.tz/mwanaglob.asp

TPN, JamiiForums na Michuzi walipowasilisha michango ya awamu ya kwanza Tanzania Red Cross Januari 15, 2010.

i1424_maafafedha.jpg


i1422_mafurikomsaada1.jpg


i1423_mafurikomsaada12.jpg


Meya Kimbisa pichani akipokea misaada ya awali; Aliwashukuru wana-Mitandao na TPN kwa jitihada zao katika janga hili na kuomba wasiache kutoa ushirikiano pindi watakapohitajika! Misaada iliyokabidhiwa ni fedha taslimu TZS 1,068,000.00 na vifaa vyenye thamani ya Tshs 1,400,000/=


Kwa kushirikiana na tovuti za Jamiiforums na Mdau wa Jamii Bw. Issa Michuzi; pamoja na kushirikiana na Mtandao wa Wanaataluma wa Tanzania (TPN) tumeandaa mpango wa kuwashirikisha Watanzania mahali popote pale walipo kuchangia katika adha hii inayowakuta ndugu zetu katika mikoa mbalimbali hasa Morogoro, Dodoma, na sasa hivi Shinyanga na hata Mwanza na kuna uwezekano wa sehemu nyingine nchini kwa kadiri siku zinavyoendelea.

Tumeamua kutumia Chama cha Msalaba na Mwezi Mwekundu cha Tanzania kwani rekodi yao katika kufika na kutoa misaada wakati wa majanga hailinganishwi na chombo au taasisi nyingine yoyote. Zaidi ya yote tumepata uhakika wa kutosha wa misaada yetu kufika kwa walengwa baada ya kuzungumza na Katibu Mkuu wa Chama hicho Mstahiki Meya (Dar) Adam Kimbisa (CCM).

Pata nakala ya mpango huo hapa:
http://www.box.net/shared/g99no7hjkg

Maelezo zaidi yanapatikana kwenye Programu ya Harambee!

Kuna tofauti kati ya kulalamika, kuhamasika na kutenda; Mwaka huu tunaenda kwenye kutenda. Hofu yangu ni kuwa yawezekana hatuko tofauti sana na jamii tunayotaka kuiongoza kuleta mabadiliko.

Nafahamu ni rahisi sana kwa wana JF kutupa lawama na kusikitika lakini ni vigumu mno kuamka na kutenda; lakini kuna wakati ambapo dhamira zituongoze kufanya vitu vizuri au tuombe misaada kwa Wamarekani utashangaa watakavyochangamka kutusaidia! Hili ni la kwetu na ningependa kuona ni jinsi gani sisi wenyewe tunaweza kufanya kitu.

Nimezungumza na Meya Kimbisa na nimepata baraka zake za kushirikiana na Red Cross TZ kwa ajili ya lengo hili. Tutawapa update baadaye leo tukishakamilisha modalities of what need to be done and by who and how. Silali leo.

=============================

JINSI YA KUCHANGIA:
Tumebuni njia mbalimbali za kuweza kuchangia vitu kama vyandarua, maboksi ya maji safi, nguo, madawa (ambayo hayajapita muda au kufunguliwa), mahitaji ya watoto na kina mama n.k.

A: MOJA KWA KWA MOJA KWA CHAMA CHA MSALABA MWEKUNDU
1. Peleka msaada wako moja kwa moja kwa Chama cha Msalaba Mwekundu kilicho karibu nawe. Kupata taarifa za Chama cha Msalaba Mwekundu wasiliana nao:
P.O. Box 1133
Dar es Salaam
Simu: (00255) (22) 215-0330/ 215-1839/215-0843 Email: logistics@raha.com

B: KUTUMIA MTANDAO WA WANATAALUMA WA TANZANIA (TPN).
Hivyo TPN itakusanya michango yetu kwa njia mbalimbali hapa chini na kuiwasilisha kwa TRCS na kutoa taarifa za mara kwa mara za maendeleo ya kampeni hii.

2. Kuingiza Benki au kuhamishia fedha benki(bank deposit and transfers):
· Jina la Akaunti: Tanzania Professionals Network,
· Jina la Benki: CRDB Bank ; Tawi: Lumumba
· Jiji: Dar Es Salaam; Nchi: Tanzania
· Swift Code: CORUTZ TZ
· US $ (Fedha za kigeni) A/C No: 02J1 007 608 900;
· TZS A/C No: 01J1 007 608 901

C: KUTUMIA MITANDAO YA SIMU
3. M-Pesa (Vodacom): 0768 777 888
4. Z-Pesa (Zantel): 0773 88 18 88
5. Zap (Zain) 0784 00 88 99

6. Michango ya kutumia makato ya kila siku ya Airtime za simu:
"Changia Shs 150 kwa siku kwa waathirika wa mafuriko. Tuma SMS yenye neno TPN kwenda 15522. Utakatwa Shs 250 kujisajili. Kwa maelezo zaidi wasiliana na 0715 740 047.

7. Western Union - Tuma kwa jina la: Mr. Emmanuel Mmari; TPN Finance and Administrative Manager; Dar Es Salaam; Tanzania. Tuma nakala ya MTCN kwa president@tpn.co.tz, info@jamiiforums.com na mwanakijiji@jamiiforums.com ili kuweka rekodi sahihi.

8: Michango ya vitu mbalimbali: Ofisi za TPN - Barabara ya Nyerere; Jengo la TOHS; Ghorofa ya kwanza, karibu na TBC (RTD) Radio. Piga simu 0715 740 047 kwa kupata msaada wa kuja kuchukua vitu kama huna usafiri.

M. M. Mwanakijiji
 
Mkuu wangu Omwana,

Ukweli ni kuwa siku za nyuma tulijaribu sana kuwafahamisha members kuwa JF haiendeshwi kwa fedha za watu flani bali kwa kujitolea.

Tukatanabaisha wazi kuwa wanachama na wote wenye mapenzi mema inabidi watambue kuwa tuna mzigo mkubwa wa kubeba kwa niaba yao.

Nyakati hizo tulikuwa na wanachama waliojisajili karibia 2,000 hivi na tukasema endapo kila mwanachama (aliyejisajili) angechangia Tshs 10,000/= basi ilimaanisha kuwa tungepata Tshs 20,000,000/= ambayo kwa wakati huo ingetosheleza kuiendesha JF kwa karibia mwaka mzima bila wasiwasi.

Maisha yakabadilika, Server tuliyokuwa nayo ilikuwa ndogo sana kumbe kulinganisha na uhitaji wa watanzania, balaa lilionekana wazi Mwezi Februari 2008 pale Mhe. Lowassa alipokuwa akijieleza Bungeni... Server ikachemsha kubeba mzigo mkubwa.

Kwa wakati huo tukaona ni vema tukaangalia namna ya kuweza kuwashirikisha wanachama juu ya ugumu tunaokumbana nao... Tukalazimika kununua server kubwa zaidi mbili na zenye back up za kila baada ya masaa 6 kwa nyakati tofauti.

Hilo likasaidia japo kwa gharama ambazo zilitoka mfukoni mwa mwanachama mmoja! Ndiyo, kulipia server hizo kila mwezi ni $940 na ameendelea kufanya hivyo kwa imani kuwa kuna siku mambo yataenda sawa.

JF inahitaji SANA michango ya watanzania na wote wenye mapenzi mema.

Kuna wanachama ambao humu mnawaona wana usernames ambazo ni bolded, hawa ni Premium Members. Hawa walau wamechangia kwa kiwango cha kuanzia $5 na wawili walau $300 tangu JF inaanzishwa mwaka 2006 (ikijulikana kama JamboForums).

Tangu JF inaanza (2006) mpaka sasa Januari 9 2009, tumekwishapokea jumla ya US$ 1,450/= toka kwa wanachama waliojisajili na wasiojisajili.

Wengi wa waliohitaji kuchangia walikuwa wanatuma barua pepe nasi tunawapa maelekezo juu ya namna ya kutufikishia michango hiyo.

Ukweli ni kwamba kwa wasio wanachama wa JF wakiwa wanasoma hapa wanaona matangazo mengi ya Google kuliko wanachama waliojisajili.

Dhamira yetu si kuweka matangazo haya ya Google kwani hayaingizi kwa kiwango kikubwa hivyo, watu hawabonyezi matangazo hayo na hivyo income yake inategemea pale mtu atakapokosea akabonyeza tangazo ndipo tupate vijisenti kidogo kwa clicks hizo. Gharama za uendeshaji bado zinatoka mfukoni mwa mtu mmoja mpaka sasa na baadhi ya Premium Members ambao wameendelea kuona umuhimu wa kufanya hivyo.

Mpaka sasa JF ina wanachama waliojisajili karibia 8,000. Endapo waliojili hawa wangechangia walau Tshs 10,000/= kwa mwaka basi inamaanisha JF ingetengeneza Tshs 80,000,000/= kwa mwaka na hivyo tusingeweka matangazo KABISA na tungejitahidi kupata moderators ambao watakuwa wanalipwa kwa kazi yao na wangeifanya kwa umakini mkubwa zaidi.

Ukiangalia katika historia ya Forums nyingi, huwa zinashindwa kuhimili traffic inapokuwa kubwa kutokana na servers kuhitaji umakini zaidi na Forum owners hujikuta wanaona ni mzigo usio na faida hivyo forums hizo kufa.

Tumshukuru Maxence kwa kuendelea kulipia gharama hizi kila mwezi kwa kujitolea mpaka sasa huku akilipia na Chat Server (IRC Server).

Wapo wanachama kama Ogah, Nyambala, SteveD, FairPlayer, Mchukia Fisadi na Phillemon Mikael ambao huchangia walau kila wanapopata wasaa... Hawa nao wamesaidia kwa kiwango kikubwa katika jitihada za kuhakikisha JF inakuwa hewani. Bila kuwasahau wadau waliochangia walau $200 hivi initially kama Mtanzania, Field Marshal ES na Halisi.

Ninachoamini binafsi ni kitu kimoja, Tshs 5,000/= kwa mwaka inawezekana kabisa kwa watanzania tulio na uwezo wa kuingia mtandaoni. Na uzuri, benki zetu Tanzania zinaruhusu mtu ku-deposit Tshs 5,000/= kama kiwango cha chini.

Endapo kuna mwanachama anaguswa (kutoka moyoni) na angependa kuiwezesha JF kuendelea kusimama imara na kufanya vema zaidi bila mizengwe ya kifedha, basi anaweza kukubali kuchangia Tshs 5,000/= walau kwa mwaka.

Benki zetu (hapa naongelea NBC na CRDB kwa haraka) hazikulazimishi unayetuma hela kuandika jina lako la kweli bali lile ambalo ungependa mpokeaji alitambue.

Kwa walio Tanzania wanaweza kuichangia JF kwa kutuma katika akaunti za NBC au CRDB.

Akaunti ambazo tangu awali tulipendekeza zitumiwe ni za Maxence Melo (as the JF Founder) na tukawaomba wanaotuma waandike Nicks za kuweza kutanabaisha kuwa wao ndio walotuma.


=================================



Michango inaweza kutumwa kwa njia kuu nne:


1. Kwa walio nje wanaweza kutumia PayPal au Credit Cards au Debit Cards kwa kufuata link hii ( https://www.jamiiforums.com/payments.php) iliyo kwenye sahihi yangu (linapoonyesha dole gumba) na pindi mchangiaji anapoweka chochote tunakuwa notified nasi tunafanya kuwasiliana na mhusika ili aweze kupandishwa kwenda katika group la Premium Members.

Paypal users:

Send via email - macdemelo@gmail.com moja kwa moja itafika na utaarifiwa ndani ya dakika 60 kuwa mchango wako umepokelewa.

2. Njia ya pili ni kutumia Western Union au Money Gram na kutuma kwenda kwa Maxence Melo Mubyazi wa Dar es Salaam.

3. Njia ya tatu ni kutumia Bank accounts za Maxence kama ifuatavyo:

NBC:

Acc #: 033201064359
Jina: Maxence Melo Mubyazi

CRDB:

Account Name: Maxence Melo Mubyazi
Bank: CRDB Pugu Road Branch
Swift Code: CORUTZTZ
Acc No: 01J2092391800

4. Njia ya nne:

Unaweza kutuma recharge vouchers za tiGO, Zain, VodaCom au Zantel kwenda kwa Maxence - 0713444649 naye atakufahamisha kuwa kazipokea.
 
Mdada it takes more than kufua na kupika to win a man's heart. Kma unaweza sogea dar ukabe rofu otherwise utaishia tu kudhani anakupenda we na mwanao.
Just curious, tangu mwanao akiwa class one na sasa yuko form three!!!! hakuna ndoa hapo, move on. let the truth be told!
 
Mdada it takes more than kufua na kupika to win a man's heart. Kma unaweza sogea dar ukabe rofu otherwise utaishia tu kudhani anakupenda we na mwanao.
Just curious, tangu mwanao akiwa class one na sasa yuko form three!!!! hakuna ndoa hapo, move on. let the truth be told!

THATS VERY TRUE CARMEL!!!
wat is holding the guy for all these years jamani?? hiyo distance yenyewe ni kikwazo tosha, alafu bado mtu uwe na mategemeo.
(huyo mwanaume naye si amwambie mama wa watu nyeupe na nyeusi tu)
 
Omwana!! mmependana tangu mtoto akiwa class 1 sasa yuko form 3!
Kwa mahesabu ya haraka haraka hiyo ni miaka kumi. if am no wrong!
Jaribu kukaa chini na kufikiria kuhusu hilo.. 10yrs still in relationship!! STUKA OMWANA.
secondly, uko Mwanza yeye yuko Dar!! Naomba katika hili tupo data kamili, How often do you visit each other? ukinijibu hili Tunaweza kushauriana vizuri dadaangu.
 
Paka Jimmy, mbona ghafla watoka nje ya mada. Toa mawazo kumsaidia huyo kijana/dada anayeomba ushsauri, please!!!!! Moderator naomba, hili bandiko la kaka Paka Jimmy ulipeleke kunakohusika kwenye michango kwa ajili ya wana Kilosa!!!
 
THATS VERY TRUE CARMEL!!!
wat is holding the guy for all these years jamani?? hiyo distance yenyewe ni kikwazo tosha, alafu bado mtu uwe na mategemeo.
(huyo mwanaume naye si amwambie mama wa watu nyeupe na nyeusi tu)
Kuna mambo mengine magumu kuyasema by word, and the expectation is that, mhusika anatakiwa asome alama za nyakati. ningekuwa mi ndo huyo dada ningeshasepa, unawezakuta huyo jamaa ana mke na watoto kabisa. na kwa ufupi jamaa ni msanii period!
 
Alishafariki


ooh so sorry jamani kwa hili

ila huyu bwana from me ni kwamba huenda ana mke mwengine huku Mwanza. Kwa nini usihamie kabisa huko kwake mkaishi pamoja ukajua moja kuliko kukaa mbali2 na huku hamjafunga ndoa?
 
Upendo wa kweli angeubadilisha kuwa NDOA!

NINA MASHAKA NA HUKO KUKUPENDA KWAKE!

Miaka hiyo karibia 7 anakuzingua tu, huoni kuna mambo fulani inaendelea?

Tena ingekuwa bora hata mngekuwa mnakaa pamoja, at least ungekuwa na uhakika kwamba unammiliki, lakini yeye Dar, wewe Mwanza....%$&***#network searching!

PJ nimecheka sana hapo kwenye red!!!
Dada akili mkichwa.
 

Similar Discussions

0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom