TRA Muheza na DC kuna nini?

Scaramanga

JF-Expert Member
Aug 19, 2020
419
572
Nimesiiliza sana clip ya DC wa Muheza na mpaka sasa nimeshindwa elewa kuna nini. Kwanza nikiri mimi nafanya biashara japo siyo kubwa ila nakumbuka kama sikosei ilikuwa sikukuu ya Iddi Mh Rais alisema baadhi yetu wafanyabiashara tumeanza kuiibia Serikali kwa kudanganya na kukwepa kodi.

Kila nikifikiria treni iliyoanza safari Dar Dodoma, nikiwaza ndege ya ATCL ya mizigo na abiria, niliwaza bwawa la mwalimu Nyerere nawaza mno tunaenda wapi. Maana vyote hivyo najua ni kodi yangu na wewe mwenzangu hata kama siyo mfanyabiashara basi utakuwa umechangia hata kwa kununua soda.

Leo DC ambaye ni mmoja wa wakusanya kodi maana ni moja ya kazi yake kama nitakuwa nimekosea mntanisahihisha maana najua tunakutanaga vikao vya kushauriana kodi wilaya yeye anasimamia na mkoa ni Mkuu wetu wa Mkoa.

Pili ni mwenyekiti wa kamati ya ulinzi na usalama wilaya. Nilitegemea hao TRA ambao anasema anawajua wanapindisha mambo angekuwa kashawashughulikia kisheria ila kuja na kuongea vile mbele ni kama kuna kamgao kakokosa.

Ila kama yeye ni msimamizi wa makusanyo yote ya wilaya iwe TRA au halmashauri akishaongea vile tutegemee ushirikiano utakosekana kati yake na TRA au wananchi tutakosa imani na chombo hicho cha mapato. Mtazamo wangu alishindwa nini kuwaita hao wawili yaani meneja wa TRA na huyo mama ofisini kwake akajua mbichi na mbivu?

Anasema mnapindisha sheria ila kuwashughulikia mnakomaa sasa alitaka wazidi kupindisha sheria kweli badala ya kuwanyoosha wafate sheria yeye anataka wapindishe zaidi. Au ni biashara yake hata nimeshindwa muelewa.

Mama amewaomba wamsaidie ila hakumaanisha kuwa kukiwa na makosa upande flani wasiguswe. Mimi na elimu yangu hii najua sana kuwa kodi TRA wanatutoza kulingana na mzunguko na siyo mtaji hivyo kuwa na mtaji wa m3 haimaanishi usilipe kodi je ameuliza kiasi alichoingiza huyo mama? Mtu anakuambia kanunua bidhaa za m sijui 82 je ulimuuliza wapi alikozipeleka? Kama manunuzi ni 82 umemuuliza ngapi alipata naamini angeangalia rekodi ya efd japo sina utaalamu ila mimi huwa nina rekodi za ile ripoti ya siku huwa natoa kopi natunza.

Najiuliza hivi TRA wakitokea na ushahidi maana mama aliamua ongea yake upande mmoja ikibainika yule mfanyabiashara mwenzetu kachemka DC itakuwaje dada yangu? Hivi tra na nyinyi mnajisikiaje na hii clip ya kuwa m3 mtu halipi mbona sisi wengine tumeanza na m3 na tunalipa kodi au kwa kuwa hatuna godfather?

 
Back
Top Bottom