KWELI Juhabahari (Clownfish) wana uwezo wa kujibadilisha jinsia kutokea dume na kuwa jike

Taarifa hii imethibitika kuwa ya kweli baada ya kufanya tathmini ya kina
Source #1
View Source #1
Source #2
View Source #2
Nimekutana na hii mtandaoni kwamba Clownfish wana uwezo wa kujibadilisha jinsia kutokea dume na kuwa jike.

Tusaidieni kuihakiki.

photo_2024-05-02_15-57-33.jpg
 
Tunachokijua
Juhabahari (Clownfish) ni aina ya Samaki wanaopatikana kwenye makundi ya rangi tofauti ikiwemo rangi nyekundu, njano, machungwa na rangi nyeusi. Samaki wadogo zaidi huwa na urefu wa kati ya sentimita 7-8 na wakubwa hufikia hadi wastani wa sentimita 17.

Samaki hawa huishi kwa kula wadudu wadogo pamoja na mazao mengine ya baharini, na kama ilivyo kwa viumbe wengine, samaki hawa hutaga mayai ambayo Clownfish mwenye jinsia ya kiume huzunguka akiyalinda muda wote kwa nidhamu kubwa kiasi cha kumfanya wakati mwingine asahau hata kula.

Uwezo wa kubadili Jinsia
Mdau wa JamiiCheck (Mkalukungone mwamba) ametaka kufahamu ukweli wa madai haya kama yana ukweli au la.

Ufuatiliaji wa JamiiCheck umebaini kuwa madai haya yana ukweli. Samaki hawa wote huzaliwa wakiwa madume.

Kwa mujibu wa Florida Museum, samaki hawa huishi kwenye makundi huku kila kundi likiwa na Samaki mmoja dume na Jike ambao ni viongozi.

Ikitokea samaki Jike amekufa au kuhama kundi, Samaki dume aliye mkubwa zaidi (Kiongozi) hujibadilisha kuwa jike ili kuendeleza kizazi na utawala.

Samaki hawa wanaopatikana kwenye makundi tofauti 30 huishi kwenye bahari ya hindi, red sea na pacific ya mashariki.
Wanataka halalisha watu kulana midume kwa midume,ukiamua fanya jua unakosea ,na usishawishi wengine ,maana hata sisi tusio mashoga wengine tunauza unga na wachawi
 
0 Reactions
Reply
Back
Top Bottom